Mafuta ya nazi yana faida nyingi kwa mwanadamu. Ni kusudio langu kushare na wewe msomaji wangu taarifa kuhusu faida mbalimbali zitokanazo na mafuta ya nazi. Fuatana name hadi mwisho wa makala haya. Kutokana na urefu wa makala haya, nitayagawa katika sehemu ya kwanza na ya pili na kama sehemu mbili hazitatosha basi nitaongeza na sehemu ya tatu.
Mafuta ya nazi yamekuwa yakitumika kama chakula na/au urembo kwa maelfu ya miaka. Mafuta ya nazi yana uwezo mkubwa sana wa kuharibu aina zote za vijidudu, virusi na bacteria hatari kwa ustawi wa afya ya mwanadamu . Mafuta haya huupatia mwili wa mwanadamu mafuta ambayo ni muhimu kwa afya ya mwanadamu.
Karibu asilimia hamsini ya mafuta ya nazi ni lauric acid ambayo ni vigumu sana kupatikana au haipatikani kabisa. Kwa ufupi mafuta ya nazi yana kiwango kikubwa cha lauric acid kuliko kitu chochote kile hapa duniani.
Mwili wa mwanadamu hubadili lauric acid kuwa monolaurin. Monolaurin ni aina ya monoglyceride ambayo ina uwezo mkubwa sana wa kupambana na nguvu ya virusi, na bacteria kama vile giardia lamblia.
Matumizi ya mafuta ya nazi eidha kama chakula ama kama urembo yana faida kubwa sana za kiafya katika mwili wa mwanadamu.
Mafuta ya nazi husagika kwa urahisi katika mfumo wa usagaji chakula wa mwanadamu na hayana madhara. Mafuta haya hayatengenezi sumu kwenye mkondo wa damu, hivyo basi ili kupata ama kuongeza nishati ya kutosha kwenye mwili wako, unashauriwa kula walau vijiko viwili vya mafuta ya nazi kwa siku au kula chakula kilicho ungwa kwa mafuta ya nazi kama vile wali au maharage.
Mafuta ya nazi yanafaa kwa aina zote za mapishi kwa sababu yana uwezo wa kustahimili joto bila kuharibika kama ambavyo aina nyingine za mafuta zinavyo weza kuharibika kutokana na joto kubwa mfano mafuta ya mzeituni.
Kama hiyo haitoshi, mafuta ya nazi huwa hayawezi kuchacha kama aina zingine za mafuta ,jambo ambalo ni faida kubwa sana kwa watu walio wekeza kwenye biashara ya utengenezaji wa mafuta ya nazi.
FAIDA ZA JUMLA ZA MAFUTA YA NAZI
1. Mafuta ya nazi huimarisha afya ya moyo wa mwanadamu.
2. Mafuta ya nazi huimarisha afya ya ubongo wa mwanadamu na kusaidia katika kuufanya ubongo wa mwanadamu kuwa na ufanisi thabiti.
3. Mafuta ya nazi yanasaidia kuuimarisha mfumo wa mmen’genyo wa chakula katika mwili wa mwanadamu na hivyo kusaidia katika kupunguza uzito au kumuepusha mwanadamu na kuwa na uzito mubwa.
4. Mafuta ya nazi yanaimarisha mfumo wa kinga ya mwili wa mwanadamu.
5. Matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya nazi husaidia katika kuifanya ngozi ya mwanadamu kuwa yenye afya njema na kumfanya muhusika kuonekana kijana.
Katika makala yanayo fuata, tuatelezea faida nyinginezo za matumizi ya mafuta ya nazi.
Comments
Post a Comment