Ushauri wa chakula na lishe wa jinsi ya kukabiliana na matatizo ya kiafya yanayoambatana na kuwa na saratani au tiba yake:
Saratani
ni ugonjwa unaotokana na seli za mwili zilizopoteza mfumo wake wa kugawanyika
na hivyo hazipo katika hali yake ya kawaida. Seli huweza kugawanyika bila
mpangilio maalum na kuharibu mkusanyiko wa seli nyingine. Seli za saratani
hutokea sehemu moja ya mwili na zinaweza kusambaa sehemu nyingine za mwili,
saratani pia husababishwa na hali ya mazingira ya vitu mbalimbali kama vile
ulaji wa vyakula vyenye visabbishi vya saratani (carcinogenic compounds), ulaji
usiofaa, unywaji 12
wa pombe, uvutaji sigara au minoni hatari,
“asbestos” lisasi (lead), uranium na zebaki.
Zipo
pia baadhi ya saratani zinazosabishwa na virusi kama hepatitis B ambayo
huleta saratani ya ini na human papiloma inahusishwa na saratani ya
shingo ya kizazi. Saratani huweza kutokea kwenye sehemu mbalimbali za mwili
kama vile mapafu, matiti ovary, kibofu cha mkojo, shingo ya uzazi, utumbo, koo,
kinywa, tezi dume (prostate), ini na ngozi.
Ulaji
unaofaa na mtindo bora wa maisha ni vigezo muhimu sana katika kuzuia saratani
na pia ni sehemu muhimu ya matibabu na kudumisha maisha bora baada ya kupata
matibabu. Matumizi ya baadhi ya vyakula huweza kuongeza uwezekano wa kupata
saratani. Uzito wa mwili ukiwa mkubwa unaweza pia kuongeza uwezekano wa kupata
baadhi ya saratani Ni muhimu kufuata mtindo bora wa maisha kwani ni bora kuzuia
kuliko kutibu.
Mambo
yanayohusiana na mtindo wa maisha yanayoweza kuchangia katika kupata saratani.
Tafiti
zinaonesha kwamba saratani za kurithi ni chache sana ila saratani nyingi
hutokana na sababu za kimazingira. Tafiti nyingi zimeonesha kuwa kiasi cha
asilimia 40 hadi 60 za saratani husababishwa na mtindo wa maisha usiofaa hasa
ulaji usiofaa na kutofanya mazoezi ya mwili. Mtindo wa maisha usiofaa
unajumuisha:
Ulaji wa vyakula vyenye nishati-lishe kwa
wingi ambavyo husababisha unene. Unene umeonekana kuhusiana na saratani ya mji
wa uzazi, matiti, figo, tezi dume, utumbo mpana na kibofu cha mkojo;
Ulaji wa nyama nyekundu kwa wingi na zile
zilizosindikwa vimehusishwa na saratani ya tezi la kiume, utumbo mpana, mapafu,
kinywa na koo;
Utumiaji wa pombe kwa wingi huongeza hatari ya kupata saratani ya mdomo, koo,
koromeo, utumbo mpana, kongosho, ini na matiti;
Ushauri
wa chakula na lishe wa jinsi ya kukabiliana na matatizo ya kiafya
yanayoambatana na kuwa na saratani au tiba yake:
Matatizo
mbalimbali yanaweza kujitokeza kutokana na hatua ya ugonjwa au aina ya matibabu
mgonjwa anayopata, hasa dawa za saratani (chemotherapy) au mionzi. Matatizo
hayo ni kama kukonda, upungufu wa
damu, kukosa hamu ya kula, kichefuchefu,
kutapika, kuhara, kukosa choo, vidonda kinywani, na matatizo ya ngozi.
Kukonda
Wagonjwa
wengi wa saratani wanapungua uzito wakati wa matibabu. Hii inaweza kusababishwa
na madhara ya saratani yenyewe, ongezeko la mahitaji ya virutubishi mwilini,
kukosa hamu ya kula, aina ya matibabu anayopata mgonjwa (dawa, mionzi au
upasuaji). Yafuatayo huweza kusaidia katika kukabiliana na tatizo hili:
Kuzingatia ulaji wa mlo kamili na ulaji
wa aina mbalimbali za vyakula;
Kuongeza ulaji wa vyakula vyenye protini
kwa wingi yenye asili ya wanyama (isipokuwa nyama nyekundu) na mimea.
Kula vyakula vilivyo laini
vilivyoboreshwa na kuongezewa vyakula vyenye protini na nishati-lishe kwa
wingi.
Kula milo midogo midogo mara kwa mara na
kuongeza asusa zenye virutubishi vingi;
Kujitahidi kula wakati una hamu yakula au
ukiwa na njaa kali na kula vyakula vile vyenye virutubishi kwa wingi;
Kufanya mazoezi kabla ya kula (kama vile
kutembea) ili kuongeza hamu ya kula na kusaidia uyeyushwaji wa chakula;
Kula taratibu, usile kwa haraka bali jipe
muda wa kutosha wakati wa kula;
Kutumia viungo vyenye harufu unayoipenda
Kutumia vinywaji kati yam lo na mlo na
sio wakati wa kula kuepuka tumbo kujaa na hivyo kushindwa kula chakula cha
kutosha; na
Kutumia vinywaji vyenye virutubishi vingi na nishati-lishe.
Upungufu
wa wekundu wa damu
Upungufu
wa wekundu wa damu huweza kusababishwa na saratani yenyewe au matibabu yake.
Pia huweza kutokana na ulaji duni hususani kula vyakula vyenye upungufu wa
madini chuma; malaria au minyoo.
Upungufu wa wekundu
wa damu huweza kukabiliwa kwa:-
Kula
vyakula vyenye madini chuma kwa wingi hususan vyenye asili ya wanyama (epuka
nyama nyekundu). Aina ya madini chuma iliyopo katika mayai na maziwa haifyonzwi
na mwili kwa ufanisi. 14
Kula matunda kwa
wingi kila siku. Tumia matunda kwa wingi kila siku. Tumia matunda yenye
Vitamini C kwa wingi pamoja na mlo kwani husaidia ufyonzwaji wa madni chuma
yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea.
Kuepuka vinywaji vyenye kafeini kama
chai, kahawa au soda wakati wa mlo kwani huzuia ufyonzwaji wa madini chuma
yanayopatikana kwenye vyakula vya mimea;
Kutumia vinywaji kama togwa, rozela,
mtindi au uji wa kimea kwan vinaongeza ufyonzwaji wa virutibishi muhimu; na
Kufuata ushauri wa mtaalam wa afya kuhusu matumizi ya vidonge vya madini chuma
na foliki aside na kutibiwa magonjwa kama vile malaria na minyoo.
Kukosa
hamu ya kula
Kukosa
hamu ya kula ni moja ya matatizo yanayoweza kusababishwa na saratani yenyewe au
matibabu yake. Yafuatayo yanaweza kuongeza hamu ya kula:
Kujaribu vyakula vya majimaji au
vilivyopondwa;
Kula milo midogo midogo mara nyingi kwa
siku badala ya kula chakula kingi kwa mara moja;
Kutumia vyakula vyenye nishati-lishe kwa
wingi;
Kuongeza asusa na kuziweka sehemu ambayo
ni rahisi kuchukua mtu anaposikia hamu;
Kunywa vinywaji mbalimbali kama juisi
halisi ya matunda, supu na vinginevyo, kidogo kidogo mara kwa mara;
Kufanya mazoezi ya mwili kwani husaidia
kuongeza hamu yakula
Kutumia viungo kwa kiasi katika chakula;
Kujaribu kubadili aina na ladha ya
vyakula unavyotumia; na
Kula pamoja na watu wengine kama familia.
Kichefuchefu
Kichefuchefu
huweza kujitokeza kutokana na matibabu ya saratani kama upasuaji, dawa au
mionzi. Mara nyingi kichefuchefu huisha baaada ya matibabu kumalizika.
Kichefuchefu kinasababisha kutoweza kula chakula cha kutosha.
Ili
kupunguza kichefuchefu yafuatayo yanaweza kusaidia:
Kujaribu
vyakula ambavyo ni rahisi kuyeyushwa tumboni kama mtindi;
Kujaribu vyakula vikavu;
Kuepuka vyakula
vyenye mafuta mengi au sukari nyingi;
Kula kiasi kidogo kidogo cha chakula
taratibu na mara kwa mara;
Kujaribu vinywaji vyenye viungo kama
tangawizi, ndimu au miti;
Kukaa sehemu yenye hewa safi na yakutosha
na kuepuka harufu ya vyakula;
Kula vyakula unavyopendelea;
Kula vyakula vilivyopoa na baada ya kula
na kujaribu kufyonza limau au ndimu;
Kusafisha kinywa kabla na baada ya kula
na kujaribu kufyonza limau au ndimu;
Endapo kichefuchefu kinatokea wakati wa matibabu ya saratani, acha kula saa
moja au mbil kabla ya matibabu kuanza, na siku ya matibabu kula vyakula visivyo
na harufu kali au viungo vikali; na
Kujaribu
kukumbuka wakati ambao kichefuchefu hutokea na kama inawezekana jaribu kubadili
mpangilio wa kula na mshirikishe daktari.
Comments
Post a Comment