Usikae karibu na mtu anayevuta sigara. Hii itakuepusha na kupatwa na magonjwa ya kuambukizwa kwa njia ya hewa. |
Magonjwa
sugu ya njia ya hewa
Aina
za magonjwa sugu ya njia ya hewa ni pamoja na ugonjwa wa pumu, saratani ya
mapafu, na mengine yanayosababishwa na kemikali zinazotoka katika viwanda
vinavyochafua mazingira kwa mfano kiwanda cha saruji, pamba na sigara.
Mambo
yanayoongeza uwezekano wa kupata magonjwa sugu ya njia ya hewa
Kuvuta
sigara, au kukaa karibu na mtu anayevuta sigara, Uchafuzi wa hewa ya ndani na
nje, kutokana na vumbi au chavua ya maua, Hewa za sumu na vumbi toka viwandan,
Unene uliokithiri, Mara nyingine magonjwa sugu ya njia ya hewa huweza kurithiwa
mfano pumu.
Ushauri
wa lishe na ulaji kwa mgonjwa mwenye magonjwa sugu ya njia ya hewa
• Endapo una ugonjwa sugu wa njia ya hewa
ni vyema kuzingatia ushauri wa mtaalamu wa afya, matibabu na kufuata kanuni za
mtindo bora wa maisha.
•
Unashauriwa kula mlo kamili na vyakula vya aina mbalimbali ili upate
virutubishi vyote vinavyohitajika kwa afya yako.
10
• Kula matunda freshi, mboga mboga zenye
rangi ya kijani, mboga mboga na matunda yenye rangi ya njano, ili kuimarisha
kinga ya mwili wako.
• Unashauriwa pia kula vyakula venye makapi
mlo kwa wingi ili kusaidia mfumo wa kusaga chakula kufanya kazi na kutoa uchafu
tumboni kwa urahisi, hali hii husaidia kuweza kupumua kwa urahisi.
• kula milo midogo midogo mara kwa mara
• Punguza matumizi ya chumvi ili kuepuka
maji kujikusanya mwilini na kusababisha kupumua kwa shida
• Ni muhimu pia kuepuka uzito uliozidi au
unene kwani huongeza tatizo la kushindwa kupumua
• Zingatia kuwa na uzito unaofaa kwa kula
chakula cha kutosha, mara nyingi mtu mwenye magonjwa sugu ya njia ya hewa
huweza kupungua uzito kwa sababu inamlazimu kutumia nguvu (nishati- lishe) kwa
kiasi kikubwa wakati wa kupumua.
•
Matumizi makubwa ya nguvu husababisha asiwe na nishati- lishe ya akiba ambayo
huhifadhiwa mwilini na kufanya mtu huyo kuwa mwembamba
Pamoja
na ushauri wa lishe mgonjwa huyu anashauriwa:
• Kuepuka visababishi na vichochezi kama
vile vumbi, kuvuta sigara, chavua, hasira, pombe na harufu kali
•
Kuhakikisha mazingira na nyumba ni safi na pia iwe na madirisha yanayoruhusu
mzunguko wa hewa.
Jinsi
ya kuzuia magonjwa sugu ya njia ya hewa
Epuka
kuvuta sigara, Epuka kukaa na mtu anayevuta sigara kwa kuzuia mtu kuvuta sigara
nyumbani na ofisini, Inapaswa kuzuia uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya watu
kama hotelini, vituo vya usafiri, kwenye vyombo vya usafiri, hosipitali,
shuleni, vyuoni, ofisini, sokoni n.k, Epuka kuchafua mazingira hasa hewa
tunayovuta. 11
Comments
Post a Comment