Skip to main content

FAIDA ZA KIAFYA ZA MBEGU ZA MABOGA

FAIDA  ZA  KIAFYA  ZA  MBEGU  ZA  MABOGA






Mbegu  za  maboga  zina  faida  nyingi  sana  kwa  afya  ya  mwanadamu.   Mbegu  za  maboga   zimethibitika  kuwa  na  kiwango  kikubwa  cha  virutubisho  vya  aina  mbalimbali  kuanzia  magnesium, manganese, shaba, protini, zinki  nakadhalika.  Zifuatazo  ni  baadhi  ya  faida  za  matumizi  ya  mbegu  za  maboga.


1.    Kuongeza  Maziwa  Kwa  Wanawake  Wanao  Nyonyesha : Kwa  wanawake  wanao  nyonyesha  matumizi  ya  mbegu  za  maboga  huwasaidia  kuongeza    kiwango  cha  maziwa  yenye  afya  kwa  watoto  wanao  nyonya.

2.    Mbegu  za  maboga  zina  zina  kiwango  kikubwa  cha  madini   ya  magnesium  ambacho  mwanadamu  anatakiwa  kukitumia  kila  siku.


3.    Mbegu  za  maboga  zina  kiwango  kikubwa  cha  madini  ya  zinc  ambayo  yana  faida   mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  kama  vile  kuimarisha  kinga  ya  mwili, kuimarisha  uwezo  wa  kuonja na  kunusa, ukuaji  wa  seli  mbalimbali  za  mwilini, kuimarisha  afya  ya  macho  na  ngozi, kulinda  na  kuimarisha  insulin pamoja  na  kuongeza  uwezo  wa  kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  wanaume.

4.    Mbegu  za  maboga  ni  miongoni  mwa  vyanzo  bora  kabisa  vya  mafuta  na  acid zitokanazo  na  mimea   ambazo  zina  faida  kubwa  sana  kwa  afya  ya  mwili  wa  mwanadamu.

5.    Mbegu  za maboga  zinasaidia  katika  kulinda  na    kuimarisha  ufanisi  wa  tezi  kwa  wanaume
 Mbegu  za  maboga  zina  faida  kubwa  sana  kwa  wagonjwa  wa  kisukari  kwani  zinasaidia  katika  kulinda, kuboresha,  kuimarisha   na  kurutubisha  insulin

6.    Mbegu  za  maboga  zina  imarisha  na  kulinda  afya  ya  moyo  na  ini
7.    Mbegu  za  maboga  zinasaidia  katika  kuboresha  usingizi. Kama  una  matatizo  ya  usingizi  unashauriwa  kutafuna  mbegu  za  maboga  pamoja  na  tunda  kidogo. Hii  itakusaidia  katika  kupata  usingizi  mzuri.
Anza  kujenga  tabia  ya  kuwa  unatumia  mbegu  za  maboga  kwa  faida  mbalimbali   kwa  afya  ya  mwili  wako  kama  ilivyo  onyeshwa  hapo  juu.   Kwa  makala  mbalimbali  za  afya  na  tiba a silia, endelea  kutembelea   : www.neemaherbalist.blogspot.com

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...