Figo |
Magonjwa
ya figo
Figo
hufanya kazi muhimu mwilini ambazo ni:-
• Kudhibiti na
kuhifadhi virutubishi na maji na kuondoa mabaki kupitia mkojo.
• Kuchuja damu ili
kuondoa mabaki ambayo ni sumu mwilini. Baadhi ya mabaki hayo ni urea, uric
acid, creatinine na ammonia.
• Kudhibiti viwango
vya electrolyte mwilini, yaani Sodium (Na+ ) na Potassium (K+). Sodium husaidia
kudhibiti wingi wa maji mwilini na pia huwezesha mawasiliano kati ya mfumo wa
fahamu na misuli (enhances commucacation between brain/nerves and muscles). Potassium
husaidia mapigo ya moyo between brain/nerves and muscles). Potassimu husaidia
mapigo ya moyo (regulates heart beats) na kazi ya misuli (muscle
function). Viwango vya kawaida kwa Sodium ni 135-145 mmol/L na
Potassimu ni 3.5-5 mmol/L.
• Kudhibiti shinikizo
la damu kupitia mfumo wa rennin-angiotension.
• Kutengeneza
kichocheo cha Erythropoietin ambacho huchochea utengenezaji wa
chembechembe nyekundu za damu.
• Kuchochea vitamin D ambayo hutumika katika
kudhibiti kiwango cha Calcium na Phosphorous kwenye mifupa.
Iwapo
mtu atapata ugonjwa wa figo ambao utaathiri figo zote mbili, kazi zote hizo
hapo juu huathirika au kushindwa kufanyika kwa ufanisi na
madhara hutokea kutengemea kiwango cha
athari. Figo zinaweza kushindwa kufanya kazi aidha kwa sababu za kipindi kifupi
(acute renal failure) au kwa sababu za muda mrefu (chronic renal failure).
Sababu
zinazoweza kufanya figo zishindwe kufanya kazi:
i)
Katika muda mfupi:
o Upungufu mkubwa wa
ujazo wa damu (kupoteza damu kwa kiasi kikubwa)
o Upungufu wa maji
mwilini kutokana na kutapika, kuhara, na homa
o Matumizi ya baadhi
ya dawa kama diuretics
o Mawe kwenye figo (kidney
stones)
o Maambukizi kwenye
figo mfano sepsis
o Uvimbe –uchungu (inflammation)
kwenye mfumo wa uchujaji kwenye figo (acute glomerulonephritis)
o Uvimbe mkubwa wa
tezi dume (prostatic hypertrophy)
o Saratani ya tezi dume (prostate cancer)
ii)
Katika muda mrefu
o Kisukari
kisichodhibitiwa
o Shinikizo kubwa la
damu lisilodhibitiwa
o Uvimbe-uchungu wa
kudumu kwenye mfumo wa uchujaji wa figo(chronic glomerulonephritis)
o Mawe kwenye figo
o Magonjwa ya tezi dume (Prostate disease)
Dalili
za ugonjwa wa figo:-
Mwanzoni,
ugonjwa wa figo hauoneshi dalili yeyote. Mara utendaji kazi wa figo
unapopungua, dalili hujitokeza kuendana na udhaifu wa kudhibiti maji na electrolyte
mwilini; kuondoa mabaki mwili; kutengeneza erythropoietin ambayo huchochea
utengenezaji wa chembechembe nyekundu za damu, na pia udhaifu wa kuchochea
Vitamini D ambayo ni muhimu katika kuweka viwango sahihi vya
calcium-phosphorous kwenye mifupa, misuli na neva.
•
Dalili za mwanzo ni kama:-
o Kudhoofika,
o Kuchoka mara kwa
mara
o Kukosa nguvu,
o Kukosa
pumzi/kupumua kwa shida
o Kuvimba mwili (hasa
usoni), na
o Homa isiyokuwa kali
Hali
hii isipogundulika mapema huweza kusababisha hatari ya kupoteza maisha.
• Udhaifu wa kutoa Sodium (Na+)
mwilini husababisha wingi wa Sodium mwilini (hypernatremia) ambao huambatana na
kujaa kwa maji mwilini (generalized oedema) kuongonzeka uzito ghafla, ongezeko
la shinikizo la damu, kushindwa kupumua mwisho husababisha ugonjwa wa moyo
(congestive heart failure).
• Udhaifu wa Potassium (K+) mwilini
husababisha wingi wa potassium mwilini (hyperkalemia) ambao husababisha misuli
kukosa nguvu au kuwa dhaifu na mapigo ya moyo kuenda ovyo ovyo (arrhythmias) na
ikizidi huweza kusababisha kifo cha ghafla.
• Kushindwa kutolewa kwa urea mwilini
husababisha uharibifu kwenye ubongo (encephalopathy).
• Udhaifu kwa ujumla husababishwa na upungufu
mkubwa wa damu ambao husababishwa na kushuka kwa uwezo wa figo kutengeneza erythropoietin
hivyo chembechembe nyekundu za damu kupungua.
• Kukosekana kwa uwiano unaotakiwa kati ya phosphorous
na calcium huweza kufanya mifupa kuwa miepesi kuvunjika.
Ushauri
wa lishe na ulaji kwa mtu mwenye ugonjwa wa figo
Ulaji
wa mtu mwenye ugonjwa wa figo unapaswa kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwani figo
haziwezi tena kutoa mabaki ya protin, maji, chumvi na potassium kwa urahisi
inapozidi mwilini. Vyakula vyenye chumvi na potassium nyingi viepukwe ikiwa ni
pamoja na kuzingatia mambo yafuatayo:
Mambo
ya kuzingatia katika ulaji:-
• Punguza kiasi cha nishati-lishe. Kiasi cha
nishati-lishe na protini kinapozidi mwilini huzipatia figo ambazo zimeathirika
kazi kubwa.
•
Punguza kiasi cha vinywaji/vimiminika- ili kupunguza kujaa kwa
maji mwilini ambako husababishwa na kushindwa kwa figo kutoa maji mwilini. Maji
yakizidi mwilini husababisha kushindwa kupumua, shinikizo kuwa la damu, kuvimba
mwili na huweza kusababisha
ugonjwa wa moyo (heart failure). Dhibiti
ongezeko la uzito wa mwili kwani huweza kuonesha kuwa maji yamezidi mwilini.
• Punguza kiasi cha sodium: Kiasi cha maji
mwilini hudhibitiwa na sodium. Pale sodium inapozidi mwilini husababisha
maji kubaki mwilini. Hali hii huweza kusababisha ongezeko la uzito ghafla,
kuvimba kwa viungio vya mwili, shinikizo kubwa la damu, kushindwa kupumua na
huweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Vyakula vyenye sodium kwa wingi ni vyakula
vilivyosindikiwa kwa chumvi (nyama, samaki, soseji, bacon). Jenga tabia ya
kutoongeza chumvi kwenye chakula wakati wa kula.
• Punguza kiasi cha potassium: Madini ya potassium
yanapozidi mwilini husababisha misuli kuwa dhaifu na mapigo ya moyo
kubadilika na yakizidi sana hueza kusababisha kifo cha ghafla. Ni muhimu
kudhibiti kiasi cha potassium kwa ukaribu. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi
kikubwa ni pamoja na maparachichi, ndizi mbivu, maboga, machungwa, pichesi,
peasi, matunda yaliyokaushwa na maharagwe. Vyakula vyenye potassium kwa kiasi
kidogo ni pamoja na zabibu, machenza, mahindi mabichi, cauliflower,
na matango.
Unaweza
kupunguza kiasi cha potassium kwenye chakula kwa kuchemsha na kumwaga maji za
ziada.
Kiasi
cha potassium kinachoshauriwa kwa siku kwa mtu wa kawaida ni gramu 4.7 (milligram
4,700). Kwa mgonjwa wa figo inashauriwa gramu 1.5-2.7 (milligram 1500-2700) kwa
siku na kila mlo asizidishe gramu 0.25 (miligramu 250).
• Punguza kiasi cha phosphorus
Uwiano
wa calcium na phosphorus mwilini ni muhimu kuwezesha afya njema ya mifupa,
misuli na neva. Phosphorus inapozidi mwilini mifupa huwa myepesi kuvunjika
(brittle) na rahisi kuvunjika. Hii inatokana na mwili kutoa calcium kwenye
mifupa vyakula ambavyo vina phosphorus kwa wingi ni pamoja na maziwa na mazao
yake, nyama, shellfish, vyakula amvavyo havijakobolewa, maharage, karanga,
korosho na chokoleti.
Vitamini na madini
ya nyongeza
Wagonjwa
wa figo huhitaji vitamin na madini ya nyongeza kutokana na kutokula aina
mbalimbali za vyakula na hivyo kuweza kusababisha
upunfugu
wa baadhi ya virutubishi. Damu inapochujwa (dialysis) pia huondoa vitamin
kwenye damu. Virutubishi vya nyongeza vitolewe kwa mgonjwa wa figo kwa ushauri
wa daktari.
Comments
Post a Comment