CR7 akiwa na watoto aliowapa msaada |
CR7 |
CHRISTIANO RONALDO ASAIDIA WATOTO WENYE UPUNGUFU WA DAMU.
SUPASTAA Christiano Ronaldo ameweka kando mambo ya ndani ya uwanja na kuonyesha uungwana mkubwa kwa kusaidia watoto wenye matatizo ya upungufu wa damu. Fowadi huyo wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno aayepewa nafasi kubwa ya kutwaa tuzo ya Ballon d’Or Januari mwakani, alikwenda kwenye Studio za Cadena Cope, ambapo watoto wane wenye matatizo hayo walikuwa wakimsubiri. Staa huyo mwenye umri wa miaka 28 pia aliwapa watoto hao kila mmoja jezi yake ya Real Madrid iliyokuwa imeandikwa “ Ronaldo 7 “ mgongoni na kasha akapiga nao picha ya pamoja.
“ Siku zote nipo tayari kusaidia watoto” alisema staa huyo alipozungumza na 101greatgoals.com.
“ Kama nitashinda Ballon d’ Or , watoto wote nyie mtakuja kwenye sherehe yangu ‘. Ronaldo alihudhuria tukio hilo la kuwahamasisha watu kuchangia damu kwa ajili ya watu wenye matatizo ya upungufu wa damu.
Comments
Post a Comment