Mlo Kamili |
Magonjwa
sugu yasiyo ya kuambukiza yanaweza kuzuiwa au kupunguzwa kwa kufuata mtindo
bora wa maisha. Mtindo bora wa maisha ni muhimu katika kuendeleza na kudumisha
afya ya mtu na kuzuia maradhi, hususani magonjwa sugu yasiyo ya
kuambukiza.Mtindo bora wa maisha ni ule unaozingatia ulaji unaofaa, kufanya
mazoezi ya mwili, kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku,
kuepuka matumizi ya pombe, na kuepuka msongo wa mawazo.
Ulaji
unaofaa:
Ulaji
unaofaa hutokana na kula chakula chenye mchanganyiko wa angalau chakula kimoja
kutoka katika makundi matano ya vyakula na kupunguza kiasi cha mafuta, chumvi,
na sukari kinachotumika.
Ulaji
unaofaa unatakiwa kuzingatia mahitaji ya mwili kutokana na jinsi, umri,
mzunguko wa maisha (mfano utoto, ujana, uzee), hali ya kifiziolojia (mfano
ujauzito, kunyonyesha), kazi au shughuli na hali ya afya.
Ulaji
unaofaa huchangia katika kudumisha uzito wa mwili unaotakiwa na kupunguza
maradhi, yakiwemo magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
Mambo
ya kuzingatia ili kufanikisha ulaji unaofaa:
• Kula mlo kamili mara tatu kwa siku.
• Kula matunda na mboga mboga kwa wingi
kila siku.
• Kula vyakula venye makapi mlo kwa wingi.
• Epuka kutumia sukari nyingi.
• Epuka kula vyakula venye chumvi nyingi.
• Kunywa maji safi, salama na ya kutosha
•
Kula asusa zilizo bora kilishe.
Kufanya mazoezi ya mwili :
Ni
muhimu kwa binadamu wote, mtoto au mtu mzima, mnene au mwembamba, mgonjwa au
mwenye afya njema kufanya mazoezi kwani husaidia mifumo mbalimbali ya mwili
kufanya kazi kwa ufanisi. Mazoezi hupunguza uwezekano wa kupata saratani,
ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo, na shinikizo kubwa la damu.
Mazoezi
husaidia pia katika kuzuia ongezeko la uzito wa mwili, kupunguza msongo wa
mawazo, na pia huboresha afya ya akili ikiwa ni pamoja na kuboresha uwezo wa
kufikiri, kuelewa na kukumbuka. Inashauriwa kufanya mazoezi ya mwili angalau
kwa dakika 30 kila siku, yaani mazoezi yanayotumia nguvu kiasi kama kutembea
kwa haraka.
Anza
kwa kutembea kwa muda mfupi, na baadaye unaweza kuongeza muda hadi dakika 60
kila siku, ukishindwa kabisa kufanya kila siku fanya angalau dakika 60 mara
tatu kwa wiki.
kuepuka
matumizi ya pombe:
Pombe
husababisha ongezeko la uzito wa mwili ambalo linahusishwa na magonjwa mengi
sugu yasiyo ya kuambukiza. Tafiti zimethibitisha kwamba pombe inaongeza sana
uwezekano wa kupata saratani hasa ya mdomo, koo, koromeo, matiti, utumbo mpana
na ini.
Tafiti
zimeonyesha kwamba pombe ina madhara mengikiafya, ikiwa ni pamoja na
kusababisha magonjwa, kupunguza uwezekano wa ini kufanya kazi vizuri, na pia
huathiri uwekaji wa virutubishi mwilini.
Endapo
unakunywa pombe kwa mwanaume inashauriwa kunywa vipimo viwili ambavyo ni sawa
na milimita 500 za bia, mvinyo milimita 200, na pombe kali milimita 50 kwa siku
. Kwa mwanamke anashauriwa kunywa nusu ya vipimo vinavyotumika kwa mwanaume.
Kuepuka
matumizi ya sigara na bidhaa nyingine za tumbaku:
Uvutaji
wa sigara, utumiaji wa tumbaku na bidhaa zake huongeza uwezekano wa kupata
ugonjwa wa moyo, saratani ( hasa za mapafu, kinywa na koo), magunjwa sugu
mengine ya njia ya hewa, shinikizo kubwa la damu na vidonda vya tumbo hivyo ni
muhimu kuepuka.
Sumu
aina ya nikotini iliyopo katika sigara huharibu ngozi ya ndani hivyo huongeza
uwezekano wa lehemu kujikusanya kwenye sehemu za mishipa ya damu
zilizoathiriwa. 21
Nikotini pia huweza kusababisha mishipa ya
damu kuziba au kuwa myembamba kuliko kawaida na hivyo kuzuia damu kupita
inavyotakiwa . Matumizi ya sigara pia huweza kuleta athari kwa wale walio
karibu na mvutaji hususani kwa mama mjamzito na mtoto.
Kuepuka
msongo wa mawazo
Msongo
wa mawazo ni hisia ambayo huweza kuamshwa na matukio mbali mbali kama vile
kufiwa na mtu wa karibu, kukabiliwa na tatizo katika( familia,maisha au
shuleni), kuwa na kazi nyingi kwa muda mrefu bila ya kuwa na muda wa kupumzika.
Hisia hizo zinaweza kusababisha hasira, wasiwasi, woga, huzuni, kuchanganyikiwa
na pia kukata tamaa. Msongo wa mawazo ukijitokeza mara kwa mara huweza
kusababisha ulaji usiofaa na mifumo ya mwili kutofanya kazi vizuri
Inashauriwa
kupunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi, kujipa muda wa kupumzika,
kushiriki katika shughuli mbali mbali kama michezo, matamasha, harusi, na pia
kupangilia vizuri jinsi ya kutumia muda wako. Jadili na mtu unayemwmini kuhusu
matatizo yako, cheka au angua kilio, zima simu yako kwa muda katika siku.
HITIMISHO
Watu
wengi tunakumbwa na magonjwa haya kutokana na kuwa na mtindo wa maisha usiofaa,
ni vyema kuzingatia mtindo bora wa maisha ili kupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
USHAURI
Ni vyema kushiriki katika michezo, na
mazoezi ya viungo.
Ni muhimu kujenga mazoea ya kupima mara
kwa mara afya zetu.
Tuzingatie mtindo bora wa maisha ili kuzuia au kupunguza uwezekano wa kupata
magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza.
Comments
Post a Comment