Watu wakioga kwenye kwenye mto wa Orimiri Jordan |
Maelfu ya watu
kutoka maeneo mbalimbali
ya nchini Nigeria
na nchi za
jirani wanaendelea kumiminika
katika mto wa
ajabu ulio batizwa
jina Orimiri Jordan
yaani Mto Yordani, kwa
ajili ya kupata
tiba ya magonjwa
na matatizo mbalimbali
yanayo wakabili.
Vyombo vya
habari nchini Nigeria, vimekuwa vikiripoti
mamia ya shuhuda
kutoka kwa watu
mbalimbali walio pokea
uponyaji kwenye mto
huo wa maajabu.
Watu wakiwa kwenye foleni ya kuingia kwenye mto wa uponyaji. |
Mmoja kati ya wazee wenyeji wa eneo ulipo tokea mto huo wa maajabu, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu mto huo wa maajabu. |
Taarifa zilisambaa
kwa haraka sana
kuanzia kwa wakazi
wote wa eneo
hilo, jimbo la Enugu
na nchi nzima
ya Nigeria.
Ilifahamika kuwa
wazee wa eneo
hilo wanasema si
mara ya kwanza
kwa mto huo
kutokea, kwani mara
ya mwisho mto
huo ulitokea ghfala
mnamo mwaka 1971
na kwamba watu
mbalimbali waliponywa magonjwa
na matatizo yao
baada ya kuoga
katika mto huo
wa maajabu.
Baada ya
kuenea kwa taarifa
kuhusu mto huo, mamia
kwa maelfu ya
wananchi wa Nigeria
na nchi jirani
wamekuwa wakifika na
kuoga katika mto
huo kwa nia
ya kupata suluhisho
la matatizo mbalimbali
yanayo wakabili.
Mpaka wakati
huu, bado hayajapatikana maelezo
yoyote ya kisayansi
kuhusu tukio hilo
la ajabu.
Kwa habari
zaidi, tembelea : http://naijagists.com/healing-river-orimiri-jordan-in-enugu-state-nigeria-fulanis-found-mysterious-pool-in-nachi-orji/
Comments
Post a Comment