Skip to main content

HII NDIO PICHA YA " JAY Z " ILIYO ZUA UTATA




Jay Z kulia, na  kushoto  ni  mtu  anaye  fanana  na  Jay Z  ambaye  picha  yake  ilipigwa  mwaka 1933  huko  Harlem, New York  City.

Picha  hii  imepigwa   mnamo mwaka  1933  kwenye  kitongoji  cha   Harlem huko New York , Marekani.


Picha  iliyo  pigwa   huko  Harlem mwaka  1933  inayo  muonyesha  mtu  anaye  fanana  na  kushabihiana  na  Rapper  Jay Z kwa  kiasi kikubwa  sana.

Katika  picha  hii   anaonekana  mwanaume    anaye  fanana   na  kushabihiana  na  Rapper  Jay Z kwa  kiasi  kikubwa  sana.

Picha  hii  iliyo  tolewa  na   maktaba  iitwayo  Schomburg  Centre  iliyopo  jijini  New York  nchini  Marekani, imezua  utata  mkubwa  sana  miongoni  mwa  mashabiki  wa  mwanamuziki  Jay  Z  na  muziki  wa  Hiphop  kwa  ujumla.

Picha  ya  mtu  anaye  fanana  na  Jay  Z 


Baadhi  ya  watu  walio  jitokeza  kutoa  maoni  yao  kuhusu  picha  hiyo, wanasema  huenda  Jay  Z   yupo  katika  kundi  la  watu   ambao   kiimani  wanajulikana  zaidi  kama  TIME  TRAVELLER.

Aina  hii  ya  watu  imezungumziwa  katika  vitabu  vya  dini  mbalimbali.

Wengine  wanasema  huenda  Jay  Z  ni  Vampire  na    wengine  wanasema   huenda  Jay  Z  amezaliwa  kwa  mara  nyingine  tena  
Reincarnation )  kama  waaminivyo    wahindu  na  wabudha.

Wanao sema  huenda  Jay  Z ni  vampire  wanajenga  hoja  zao  kwa  ku fanya  reference  kwenye  masuala  mbalimbali  yenye  utata  yanayo muhusu  Jay  Z  kama  vile  kuhusishwa  na   secret societies  

Mmoja  kati  ya  wachangiaji  hao  alisema 

"  Usikilizeni  vizuri  wimbo  wa  Forever  Young, Jay  Z  alikuwa  anamaanisha  anacho  kiimba, huenda  huyu jamaa  akawa  ni  vampire  kweli "

Wakati  watu  wengine  wanasema, huenda  mtu  huyo  ambaye   jina  lake  halikuweza  kujulikana,  anaweza  kuwa  ni  babu   wa  mwanamuziki  Jay  Z.

Na   wengine  wanasema, huenda   imetokea  tu  kama  co-incidence  kwa  sababu  wapo watu wengi  tu  ambao  hawana  unasaba  wa  aina  yoyote  ile  lakini  wanafanana  kwa  kila  kitu  kama  wasemavyo   waswahili  kuwa  “ Duniani  wawili “
Wewe  msomaji  una maoni  gani  kuhusu  suala  hili ?

Comments