Skip to main content

MWANAMKE ALIYEKUWA AKIJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA, ATOA USHUHUDA MZITO KANISANI!



Maria, mwanadada  aliyekuwa  akijihusisha  na  mapenzi  ya  jinsia   moja.



Siku  ya  Jumapili  ya  tarehe  23  Machi  2014, kanisa la  The Synagogue  Church Of  All  Nations  ( SCOAN )  lilishuhudia  shuhuda kutoka  kwa  wanadada  wawil   ambao  walikuwa  wakijihusisha   na  mapenzi  ya  jinsia  moja  ambao  walikiri  kuingiwa  na   mapepo  wachafu  ambao  walikuwa  wakiwasukuma  kujihusisha  kimapenzi  na  wanawake  wenzao.

Maria Terese George  kutoka  Delta State, Nigeria  alieleza  mbele  ya  makutano  walio  kutanika  kanisani  hapo  kwamba, umasikini  uliokithiri  katika   familia  yake  ulimsukuma  kwenda  kuomba  msaada  kwa  mwanamke  mmoja  wa  makamo.

Mwanamke  huyo  aliahidi  kumsaidia  mwanadada  Maria. Ambacho  Maria  hakukifahamu  ni  kwamba, mwnanamke  huyo  alikuwa  anajihusisha  na  mapenzi  na  jinsia   moja  na  alitumia  suala  la  kumpa  msaada  kama  gia  ya  kumuweka  karibu  naye ili  amshawishi  waingie  katika  uhusiano  huo.


Maria  ambaye  kwa  wakati  huo  alikuwa  ana  umri  wa  miaka  19, anasema    Alinichukua  na  kunipeleka  kwenye  klabu  ya  usiku ambako  tulikunywa  sana  pombe.  Baadaye  alinichukua  na  kunipeleka  hadi nyumbani  kwake  kasha  akaanza  kunitomasa  na  kunipapasa  kimahaba. Kwa  kuwa  nilikuwa  nimelewa, name  nilimpa  ushirikiano.


Usiku  wa  siku  iliyo  fuata, Maria  ( ambaye  picha  yake  inaonekana  hapo  juu  ) akiwa  amelala  usiku, alijiwa  na  ndoto  ya  ajabu  sana. Anasema

  Mwanamke  aliye  nusu  uchi  aliniijia  katika  ndoto  na  kuanza  kunirisha  wali, mchemsho  na  nyama .”

Baada  ya  kuamka, Maria  alipoteza  hisia  zake  za  kimapenzi  kwa  wanaume  na  akaanza  kuwatamani  wanawake  wenzake.

Anasema     Hivyo  ndivyo    pepo  la  usagaji  lilivyo  niingia.  Nilijigundua  kuwa, kila   nilipokuwa  nikimuona  mwanamke  mwenye  umbo  lililo  jazia, ilikuwa  lazima  nivutiwe  na  kumtamani  kimapenzi. Baadaye  nikawa  msagaji  aliye  kubuhu  Anakiri  mbele  ya  makutano..

Baada  ya  muda  mfupi, mwanamke  yule  yule aliyemuingiza  kwenye usagaji, akamuingiza   kwenye  mtandao wa  kufanya  biashara  ya  kuuza  miili  yao  kwa  wanaume  matajiri. Mwanamke  huyo  alimwambia  kuwa, atafanikiwa  na  kuwa  tajiri  kwa  biashara  hiyo  ya  kuuza  mwili  wake.

  Kila  nilipohitaji  pesa, nilikwenda  kulala  na    wanaume  matajiri, wanasiasa  na  wafanyabiashara, lakini  kama  nikitaka  kuenjoy  sex  nilikuwa  naenda  kulala  na  wanawake  wenzangu “


Biashara  ya  ukahaba  ilimfikisha  Maria  katika  nchi  jirani  ambako  aliendelea  kutopea  katika  maisha  yakidhalili. Hata  hivyo  pesa  alizokuwa  akizipata  kutoka  na  biashara  hiyo  hazikuwa  zikikaa, kwani  alikuwa  akizitumia  kwa  starehe  mbalimbali.
Baada  ya  miaka  kadhaa  ya  kuishi  maisha  ya  ukahaba  na  frustrations, Maria  aliamua  kurejea  nyumbani.

  Niliporudi  nchini, nilianza  kuwatafuta  wanawake  niliokuwa  ninashiriki  nao  mapenzi  ya  jinsia  moja. Maria  anasema kila  aliokuwa  akiwapigia  walikuwa wakimcheka  na  kumwambia  kuwa  wameolewa  na  wana  watoto  tayari.”
Maria  alipigwa  na  butwaa!.

Hakufikiria  kama  ingewezekana  kwa  mwanamke  kuacha  usagaji.

  Nilichanganyikiwa  sana  na  kuwauliza  walimaanisha  nini. Wanawake  wote  wane, kila  mmoja  kwa  wakati  wake  waliniambia  kuwa  walikwenda  kwenye  kanisa  la  T.B JOSHUA  kwa  ajili  ya  kufanyiwa  deliverance.,”   kwa  mshangao  wa  waumini  walio kuwa  wakimsikiliza, mwanadada  Maria  alisema    Inawezeka   labda  waumini  wakawa  hawafahamu  kuwa  kuna  idadi  kubwa  sana  ya  wanawake  wasagaji  ambao  wakuja  kuwa  delivered  hapa  SCOAN “


Baada   ya  kusikia  hivyo  kutoka  kwa  rafiki  zake  hao, Maria  alifanya  uamuzi kutoka  ndani  ya  moyo  wake kwamba,  atakwenda  katika  SCOAN  kwa  ajili  ya  ufanyiwa  deliverance .

Usiku  wa  siku  hiyo, Maria  akiwa  amelala  usiku  wa  manane  alijiwa  na  ndoto  nyingine  ya  ajabu. Anasema :

  Yule  mwanamke  aliye nitokea  ndotoni  akiwa  nusu  uchi, alinijia  tena  na  kuniambia, unadhani  unaweza  kuniacha  mimi!  Nenda  kachukue  kisu  na  ujiue!

Asubuhi   yake, Maria  alidamkia  kwa  kanisani  kwa  T.B JOSHUA  kwa ajili  ya  kufanyiwa  deliverance.

Wakati  wa  ibada  ya  siku  ya  Jumapili  ya  tarehe 16 MACHI  2014  mmoja  kati  ya  wazee  wa  kanisa   la  SCOAN   alimfanyia  maombi  Maria  ambaye  anasema  kuwa  ali hisi  kufunguliwa  kutoka  katika  kifungo  alichokuwa  nacho, kwani  alihisi  nguvu  ya  ajabu  sana  ikiingia  katika  nafsi  yake, na kumfungua  katika  kifungo  alichokuwa  amefungwa.

“ Sijawahi  kufeel  nguvu  kama hiyo kabla. Niliwahi  kwenda  kwenye  makanisa  mengine  kwa  ajili  ya  kufanyiwa  deliverance lakini  hali  hii  haikuisha  sana  sana  ilizidi  kuongezeka “


Anasema  wakati  anaombewa  mashetani  yalipanda  na  kuanza  kutoa  sauti  za  ajabu    kupitia  kinywa  chake.

Baada  ya  kufanyiwa  deliverance  Maria  alitoa  ushuhuda  kwamba, amefunguliwa  kabisa :

  Sasa  sina  hisia  tena  kwa  wanawake  wenzangu. Ninapo  muona  mwanamke   yoyote, sipati  hisia  hizo  tena. Namuona  kama  dada  yangu  au  mama  yangu. Sasa  hivi  ninajiona  kama  mwanamke   ambaye  nitakaa  na  kutulia  na mwanaume..”


Advising

Akitoa  ushauri  kwa  watu  Maria  anasema,   Pepo  la  usagaji  ni  pepo  linalo  tesa na  kusumbua  sana. Ina hitajika  neema  ya  Mungu  kulishinda 

Akitoa  maoni  yake, Mtumishi  wa  Mungu, Prophet   T.B. Joshua  alisema   Usiwachukie  watu, bali  chukia  matendo  yao.  Yesu  anawapenda  wenye  dhambi  lakini  anachukia  dhambi  zao .   Sasa  umefunguliwa, ni  wakati  sasa  wakuishi  katika  neon.   Kwa  sababu  katika  yeye  ( Yesu)  umefunguliwa  kutoka  katika  vifungo  vya  kiroho.

Nneoma Onyema  naye  alikuwa  na  historia  yenye  kushabihiana  na  historia  ya  Maria.  Akiwa  na  umri  wa  miaka  18  Nneoma  alikimbia  kijijini  kwao  na  kwenda  kuishi  katika  jiji  la  Port  Harcourt,Nigeria  akifanya  kazi  ya  ususi  kwenye  saluni.

Siku  moja,  mwanamke  mmoja  tajiri  alimfuata kazini  kwake  na  kuanza  kumsifia  kwa  uzuri  wake  wakati  akimsuka. Baadaye   mwanamke  huyo  akampa  Nneoma  pesa  ya  zaida  na kasha  kumkaribisha  kwenye   klabu  ya  usiku  ya hadhi  ya juu.   Wakiwa  kwenye  klabu  hiyo  ya  usiku, mwanamke  alimnunulia  Nneoma  pombe, ambapo  kesho  yake  asubuhi  Nneoma  alijikuta  yupo  kitandani  huku  pembeni  yake  akiwapo  mwanamke  huyo  akimtomasa  na  kumpapasa

“ Baadaye  mwanamke  huyo  alinibadilisha  jina  na  kuniita  Jennifer na  kunipeleka  kwa  mwanaume  ambaye  alinichora  tattoo  ya  mapenzi  mgongoni,”

Nneoma  aliendelea  kulielezea  kanisa  kuwa, mara  tu  baada  ya  kufanya  mapenzi  ya  jinsia  moja  na  mwanamke  huyu, hisia  zake  za  kimapenzi  zikahamia  kwa  wanawake  wenzake.

Kazi  ya  Nneoma  ikawa  ni  ku dance  na  kustrip  kwenye  klabu  za  usiku, na  aliweza  kukaa  miaka  mitatu  bila  kuwasiliana  na  familia  yake.


Hata  hivyo  baada  ya  kushambuliwa  na  kujeruhiwa  vibaya  na  msichana   aliyemtuhumu  Nneoma   kutoka  kimapenzi  na  rafiki  wa  kike  wa  msichana  huyo,  jirani  yake  mmoja  alimshauri  aende  kwa  T.B Joshua   kwa  msaada.

  Wazee  wa  kanisa  walipo  niombea, nilihisi  kama  nimepigwa  na  shoti  ya  umeme  mwili  wangu mzima.”

Wakati  akifanyiwa  maombi, pepo  lililokuwa  ndani  ya  Nneoma  lilipo  ulizwa  wewe  ni  nani, lilijibu  “ I am the  great lesbian” na   nimekuja  kwa  ajili  ya  kutesa  maisha  ya  Nneoma.

Wakati  huo huo, kaka  wa Nneoma aliyejulikana  kwa  jina  la  Emmanuel  alisema  alifurahi  sana  kumuona  dada  yake  akitoa  ushuhuda   kanisani  kwani   tangu  alipo toweka  nyumbani, familia  ilikuwa  ikiomba  usiku  na  mchana  kuhakikisha  Nneoma  anarejea  nyumbani

  Kila  siku  nilikuwa  naweka  picha  ya  Nneoma  kwenye  screen  pindi  Prophet  T.B Joshua  alipokuwa  akianza  kufanya  maombi, na  nilishituka  sana  kumuona  kanisani  akitoa  ushuhuda   SCOAN   siku  hiyo.,”   Emmanuel   anaongeza  kuwa, alikuwa akiusikia  ushuhuda  wa  dada  yake  kwa  mara  ya  kwanza.

Naye  T.B Joshua  alito  ahadi   ya  kumsomesha  Nneoma ili kumsaidia  kuanza  maisha  yake.

In the wake of Nigeria’s recent anti-gay law, T.B. Joshua courted controversy in January 2014 when he declared that homosexuals should not be condemned.


SOURCE :  MITANDAO  MBALIMBALI  YA  KIJAMII

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...