Skip to main content

KAMA UNAKUMBWA NA MATATIZO YA KUUMWA KICHWA, HARARA, NA KIUNGULIA INAWEZEKANA MWILI WAKO HAUNA UWEZO WA KUHIMILI HISTAMINE

Mvinyo  mwekundu
Inaweza kukushangaza kuwa baadhi ya vyakula maarufu na vinavyopendwa, mathalani matunda ya jamii ya machungwa, yaani machungwa yenyewe, machenza, malimau, ndimu, na mabalungi, vinaweza kukusababishia hisia za kuumwa. Vyakula vingine katika kundi hili ni pamoja na:
• Mvinyo mwekundu;
• Jibini;
• Achari;
• Nyama ya nguruwe; 
• Mtindi; 
• Mayai; 
• Vyakula vinavyoandaliwa kutokana na viumbe wanaovuliwa baharini (sea food);
• Nyama zilizochakatuliwa kama soseji; 
• Nyama zilizokaushwa; 
• Viporo vya nyama;
• Yogurt; 
• Matunda ya jamii ya zambarau;
• Matunda yaliyokaushwa;
• Vyakula vilivyochachuliwa (fermented); 
• Spinachi;
• Nyanya – ikiwa ni pamoja na ketchup, tomato sauces;
• Rangi bandia za vyakula na kemikali za kuongeza muda wa matumizi kwenye chakula (Preservatives);
• Viungo: Mdalasini, pilipili ya unga, karafuu, nakadhalika;
• Vinywaji: Chai, Pombe;
• Chocolate, cocoa, na vinywaji vya cola ; na
• Siki (vinegar) and na vyakula vyenye siki kama vile achari, ketchup, na kadhalika.

Jibini
Hisia hizi zinajidhihirisha kwa dalili kama vile maumivu ya kichwa, kuwashwa kwa ngozi, msongo, kiungulia kikali, kubanwa kwa njia ya hewa (nasal congestion), nakadhalika. Kama mwili wako unapata hisia za kuumwa (mizio) baada ya kula aina fulani za vyakula, ikiwa ni pamoja na hivyo vilivyoorodheshwa hapo juu, inawezekana unakabiliwa na tatizo lisilojulikana sana, japokuwa linawakabili watu wengi: tatizo la mwili wako kushindwa kuhimili uwepo wa homoni ya Histamine (Histamine intolerance).
Histamine ni kemikali ya kiorganic ambayo moja ya viasili vyake ni nitrogen. Histamine ni moja ya kemikali zinazozalishwa na mwili pale kinga za mwili zinapojibu shambulizi au mashambulizi ya kitisho chochote dhidi ya mwili. Histamine hufanya kazi hii kwa kusababisha vimishipa vidogo vya damu kupanuka ili kuwezesha chembechembe nyeupe za damu, pamoja na baadhi ya protini kupita kwa urahisi, kwenda kupambana na kitisho chochote ambacho kimeuvamia mwili.
Kemikali hii hufanya pia kazi ya kuratibu baadhi ya shughuli za kifiziolojia zinazoendelea katika njia ya chakula, hasa tumboni. Histamine inafanya pia kazi kama ‘neurotransmitter’, yaani kemikali inayopokea, kukuza na kusafirisha mawimbi ya umeme yaliyobeba taarifa maalum kutoka katika seli zinazounda mishipa ya fahamu hadi katika seli nyingine katika mwili.
Kama hujawahi kuisikia dhana ya mwili kushindwa kuhimili homoni ya histamine, tambua kuwa huko peke yako. Kwa kawaida ni vigumu sana kulitambua tatizo hili la mwili kushindwa kuhimili homoni ya Histamine. Kwanza kabisa tatizo hili linazaa dalili nyingi, na mara nyingi dalili hizi hudhaniwa kuwa zimetokana na matatizo mengine kabisa ya kiafya. Madaktari wengi na wataalamu wa lishe hawajawahi kuisikia dhana hii na hivyo basi huishia kutoa matibabu ambayo hayalengi kabisa kiini cha tatizo. Ukweli wa mambo ni kwamba tatizo hili ni la kawaida sana, japokuwa halieleweki vema.
Tofauti ya mizio ya kawaida inayotokana na vyakula, na mizio inayoletwa na mwili kushindwa kuhimili Histamine!
Tatizo la mwili kushindwa kuhimili Histamine kwa kawaida husababishwa na mapungufu katika moja ya mifumo, kati ya mifumo miwili, ya vimeng’enya vinavyohusika na mchakato wa uvunjifu wa Histamine ndani ya mwili. Mfumo huu ni ule ujulikanao kama diamine oxidase (DAO). Mfumo wa pili hujulikana kama histamine N-methyl transferase (HMT). Upungufu katika huu mfumo wa DAO, ambao hupatikana katika utando unaozingira njia ya chakula (intestinal mucosa), unatajwa kuwa ndicho chanzo kikuu cha mwili kushindwa kuhimili Histamine. Ni dhahiri kwamba kuna tofauti za kimaumbile baina ya mtu na mtu, kuhusiana na utendaji kazi wa mifumo hii ya vimeng’enya. Hata hivyo inaaminka kuwa iwapo yeyote katika mifumo hii utakumbwa na mapungufu yatakayopelekea ufanye kazi kwa kiwango cha chini, basi kutakuwa na Histamine ya ziada mwilini, na hali hii itasababisha kujitokeza kwa dalili nyingi mwilini zinazoshabihiana na mizio. Miongoni mwa dalili hizi ni pamoja na:
• Kuwashwa, hususan kwenye ngozi, macho, masikio na pua (Pruritus)
• Harara kwenye ngozi (Urticaria)
• Kuvimba kwa tishu (angioedama), hususan katika uso, kinyani na wakati mwingine kwenye koo – kitu ambacho kinamfanya mtu ajenge hisia kama vile anakabwa
• Kushuka kwa shinikizo la damu (Hypotension)
• Kuongezeka kasi ya mapigo ya moyo (Tachycardia)
• Dalili zinazofanana na msongo au wasiwasi mkubwa
• Maumivu ya kifua
• Kubanwa kwa njia ya hewa na kuwa na pua inayotoa kamasi kila mara
• Macho mekundu, yanayotoa machozi, huku yakiwa na hisia za kusumbuliwa (Conjunctivitis)
• Aina tofauti tofauti za maumivu ya kichwa
• Uchovu, kuchanganyikiwa, na hisia za kukereka
• Kupoteza fahamu kwa sekunde moja au mbili 
• Kujisikia vibaya kwenye njia ya chakula, hususan kujisikia kiungulia, kuvimbiwa na hali ya kucheua maji makali ya tumboni (reflux)
Mizio inayozaliwa kutokana na mwili kushindwa kuhimili Histamine ni tofauti na ile inayoletwa na vyakula. Wakati mizio inayosababishwa na vyakula ni ya papo kwa papo baada tu ya kula, ile inayosababishwa na Histamine huja taratibu huku ikiongezeka kidogo kidogo (cummulative). Mfano wa hali hii ni kama maji yaliyoko kwenye kikombe. Kikombe kinapokuwa kimejaa kabisa, tone moja la ziada la maji linatosha kufanya maji yaliyoko kwenye kikombe yaanze kumwagika. Lakini maji yanapokuwa hayajajaa sana kwenye kikombe, kutahitajika kiasi kingi cha maji (Histamine) kabla tukio la kumwagika kwa maji yaliyoko kwenye kikombe halijachochewa kutokea. Hali hii inasababisha utambuzi wa kuwa mwili hauna uwezo wa kuhimili Histamine kuwa mgumu.
Kwa nyongeza, kushindwa kwa mwili kuhimili Histamine kuna mahusiano ya karibu sana na ongezeko la kupindukia la bakteria kwenye utumbo mwembamba (small intestine bacteria overgrowth – SIBO). Hii ina maana kwamba ukitibu tatizo hili la ongezeko la bakteria, basi moja kwa moja unaleta ufumbuzi katika tatizo la Histamine. Matabibu wengi wanaokumbatia mifumo tofauti ya tiba (integrative practiioners) wanaamini kuwa tatizo la mwili kushindwa kuhimili histamine, kimsingi linatokana na ongezeko kubwa la lililopindukia mipaka la aina fulani fulani za bakteria katika njia ya chakula. Bakteria hawa hutengeneza histamine nyingi kutoka kwenye chakula ambacho hakikusagwa vema tumboni na kupelekea njia ya chakula kuwa na kiasi kikubwa cha histamine. Ongezeko hili kubwa la histamine huufanya uwezo wa mwili kuivunja na kuiondosha kuzidiwa. Hali hii huzidi kushusha uwezo wa mwili kuihimili histamine na hivyo kupelekea mwili kujenga upinzani dhidi ya vyakula vyote vyenye histamine kwa wingi Ulaji wa vyakula hivi moja kwa moja huzalisha dalili ambazo tunazioanisha na mizio.
Nini unachpaswa kufanya kama mwili wako hauwezi kuhimili histamine Kwa kuwa vyakula vingi vina histamine na kwa baadhi ya watu bakteria walioko kwenye njia zao za chakula huzalisha kiasi kingi cha histamine kinachopekea wawe na dalili za magonjwa zinazowakumba, tatizo hili kwa kweli linaweza kuwa ni changamoto kubwa katika kulipatia ufumbuzi. Vyakula vilivyochachuliwa ni miongoni mwa vyakula vinavyoongeza uzito wa changamoto hii ukizingatia kuwa hata bakteria wazuri walioko tumboni nao pia huzalisha histamine pale wanapokutana na mazingira ya uchachu. Moja ya vipimo vyepesi vya kujua kama unakabiliwa na tatizo la mwili wako kutoweza kuhimili histamine ni kula vyakula vilivyochachuliwa.
Kwa mtu yeyote mwenye tatizo la mwili wake kushindwa kuhimili histamine, kuondoa vyakula vyenye histamine nyingi katika ulaji wake ni jambo la lazima, walau kwa muda fulani. Baada ya hapo mgonjwa anaweza kuanza kula kiasi kidogo cha vyakula hivi. Hata hivyo athari ya histamine inatofautiana kati ya mtu na mtu. Wakati baadhi ya watu miili yao haiwezi kuvimilia kiasi chochote cha histamine, baadhi huathirika tu pale wanapokula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha histamine.
Ili kuujengea mwili wako uwezo zaidi wa kuhimili histamine ni muhimu sana kuikarabati njia yako ya chakula ikiwa ni pamoja na kushughulikia matatizo yote yenye uhusiano na ‘SIBO’ kama yapo..Unywaji wa maji wa kutosha ni moja ya njia za uhakika sana katika kudhibiti ongezeko kubwa la histamine na pia kukarabati njia ya chakula. Aidha kujenga mazoea ya kutumia tembe mbili hadi tano za vitunguu saumu kwa siku , na kupunguza sana ulaji wa sukari na vyakula vya wanga uliochakatuliwa, ni vitendo ambavyo vitasaidia sana kupunguza wingi wa bakteria wabaya kwenye njia ya chakula.

CREDIT : HERBAL IMPACT

Comments

Popular posts from this blog

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

CHANZO NA TIBA ASILIA YA TONSILS

Dawa ya TONSILS ni (kugargar)  kusukutuwa maji yalokuwa si moto sana pamoja na chumvi mara 4 kwa siku yafike kooni. Pia unatakiwa usitumie pili pili manga wala tangawizi. Kwani watu wengi utasikia wanakunywa chai ya tangawizi na soup iliyojazwa pili pili manga. Kumbe unaona vizuri wakati unapokunywa lakini huwa unayavimbisha matonsils kwani baada ya nusu saa utaona unaumwa kuliko mwanzo na homa kuja juu. Uzuri kuwa unakunywa maji ya moto moto. Vile vile kuchukuwa mdomo wako na kuweka kwenye goti na kuwa unalipuliza bila kutoka pumzi mara kwa mara na kama hufikii goti lako basi unaweza kuchukuwa kanga na kufanya mfano wa mpira na kuwa unapuliza kila utakapokuwa na wakati, hii pia inasaidia. Usiwe unazungumza sana isipokuwa kwa dharura kwani ujaribu utakavyoweza upepo usipite kwenye mdomo wako. Sio lazima unywe maji baridi ndio upate Tonsils mfano A/c linapofanya kazi upepo wa baridi unapita kwenye mdomo wako basi unapata Tonsils Au wakati unapolala na A/c linafany...