Masaji
ni nini? Ni neon linalotumika kuelezea
utalaam wa kunyumbua (kubonyeza, kusugua, kukanda) ngozina misuli ya mwili.
Mtaalam
wa masaji mara nyingi hutumia viganja vya mikono lakini wanaweza kutumia sehemu nyingine za mwili
kama vidole, viwiko hata miguu ilikuleta matokeo yanayohitajika.
Pia
kunavifaa mbalimbali vilivyotengenezwa kwa mbao, plastick na baadhi hutumia
umeme.(kama vile electronic massage beds and chairs). Pamoja na vifaa vyote
hivyo mikono ya binadamu ndio inasemekana kuleta matokeo mazuri zaidi.
Hii
ni taaluma ambayo ipo tangu enzi na sehemu nyingine katika nchi za Asia unakuta kila familia ina angalau mtu
mmoja anayeweza kuifanya kazi hii kwa ustadi.
Nimewahi
kusikia sehemu za Zanzibar wakiwaita “wakandaji.”
Masaji
imewekwa kwenye kundi la tiba mbadala ingawa imekuwa ikitumika hata kwenye tiba
za kisasa (katika hospitali n.k).
Biashara
ya masaji ikijumishwa na biashara nyingine za ‘Wellness” ni ya mabilioni ya
dola vikiwemo vifaa, mavazi ya wahudumu, mifumo ya kompyuta kwa ajili ya
usimamizi wa senta na mafuta mbalimbali ya kiasili ambayo hutumika. Nchi
nyingine tiba ya masaji imeongezwa kwenye bima za afya na imekuwa ikipendekezwa
na madaktari.
Taaluma
ya masaji imekuan sana kwa sasa ambapo kuna masaji maalum kwa ajili ya vichanga
na wajamwazito.
Kwa
mfumo wa maisha ulivyo sasa na pia kutokanana kukua kwa vipato ni dhahiri
biashara ya masaji itaendelea kushamiri na kuwa muhimu katika maisha ya kila
siku.
Faida
za masaji: Masaji ina faida nyingi mwilini moja kuu ni
husaidia kuongeza mzunguko wa damu mwilini na kupelekea kutibu hali mbalimbali
hasa msongowa mawazo na msongo wa misuli.
Navyoiona
biashara ya masaji Tanzania: Kwanza inakua kwa kasi, sasa hivi
hoteli nyingi kisasa zina vitengo vya masaji. Huko angalau kuna utaratibu na
ustaarabu unaotakiwa na wahudumu wana utaalaam/ elimu kuhusu masaji.
Lakini
pia naona kuongezeka kwa watu wanaotambua umuhimu wa masaji na wanaoweza kutoa
hela ili wapate huduma hii. (Massage is not cheap).
Ukiondoa
sehemu ya hali ya juu, huku kwingine tumekuwa na sehemu za masaji ambazo baadhi
zinajitahidi kuwa za kitaalam ila nyingi zinalalamikiwa kutumiwa kama mlango wa
biashara nyingine.
Masaji
ni taaluma, unahitaji kwenda shule ili ufahamu unachokifanya kwenye mwili wa
binadamu kujua misuli ya mwili, milalo nakazi zake.
Mara
nyingi kazi ya masaji imefananishwa kama tu kitu cha kuonyeshwa halafu unajua
(look and do), hapana.
Kwa
hiyo bado suala la kuwa mfumo wa kuandaa wataalam hawa hatunao .Na kwa
kukosekana taaluma hii pia tunaona mapungufu makubwa katika masharti kwa
watoaji wa huduma hii.
Unakuta
mhudumu amefuga kucha refu, amevaa mavazi yanayoonyesha sehemu za mwili wake
n.k.
Katika
nchi zilizoendelea wataalam wa masaji (massage technicians, massage therapists ) wamekuwa wakilinda sana taaluma yao kwa
kuweka masharti ambayo hufuatwa na kila mmoja wao.
Kuna
utitiri wa watu wanaotoa huduma hii ndivyo sivyo- quacks).
Ushauri
kwa wanaoona fursa ya kibiashara
1.
Eneo lako la biashara liwe mahali ambapo ni pa kuaminika sio vichochoroni. (kwa
mfano uwe na ample parking na security)
2.
Gharamia muonekano wa kitu chako cha masaji (muonekano, vifaa, vitanda, sehemu
ya kusubiri wateja). Weka mandhari nzuri ndani ya vyumba, decorate pawe na
reception ambayo mteja atakuwa huru kusubiri. Pia uwe na receptionist anayeweza
kupokea appointments za wateja.
3.Vyumba
viwe na mpangilio mzuri,vifaa visafi shuka na mataulo. Pia hakikisha unaweka
vitanda vile maalum kwa ajili ya masaji
kama vinavyoonekana kwenye picha.
Vyumba
viwe nadhifu.
Comments
Post a Comment