Skip to main content
Faida ya juice za matunda mchanganyiko kama tiba ya mwili wa binadamu ...........SEHEMU YA PILI
Juisi ni kinywaji bora, lakini ni vyeme ukajua juisi ipi ina
faida mwilini na ipi haina faida yoyote. Katika zama tulizonazo,
kumezuka aina nyingi za vinywaji vinavyoitwa juisi, wakati si juisi bali
ni vinywaji vyenye ladha ya matunda mbalimbali.

Juisi ni kinywaji kilichotengenezwa kutokana na tunda halisi au mboga
na si mchanganyiko wa maji na kemikali nyingine zenye ladha ya matunda
na kupewa majina kama juisi ya machungwa, nanasi, zabibu, n.k. Mara
nyingi vinywaji hivyo huwekewa sukari na kemikali nyingine za kuhifahdia
(preservertives) ili zisiharibike, ambavyo kiafya havikubaliki.
Licha ya kutumia jusi halisi kama kinywaji tu, juisi pia hutoa kinga
na tiba kwa maradhi mbalimbali. Iwapo mtu atatengeneza mchanganyiko
maalum wa matunda na kutayarisha juisi maalum na kuinywa, anaweza kupata
kinga na tiba ya matatizo mbalimbali ya kiafya kama ilivyoanishwa hapa
chini:

KAROTI+ KITUNGUU SWAUMU + EPO
Juisi ya mchanganyiko wa karoti, kitunguu swaumu na epo (apple) husafisha sumu mwilini na kuupa mwili nguvu.
EPO+TANGO+FIGILI
Juisi ya mchanganyiko wa tunda la epo, tango na mboga ya majani aina
ya Figili (celery) hutoa kinga ya saratani, hupunguza mafuta ya kolestro
mwilini na huondoa hali ya kuchafuka kwa tumbo na kuumwa kichwa.
NYANYA+KAROTI+EPO
Juisi ya mchanganyiko wa nyanya, karoti na epo huboresha rangi ya ngozi na huondoa harufu mbaya mdomoni.
CHUNGWA+TANGAWIZI+TANGO
Juisi ya mchanayiko wa machungwa, tangawizi na matango huboresha ngozi na hushusha joto la mwili.
NANASI+EPO+TIKITI MAJI
Juisi ya mchangayiko wa nanasi, epo na tikitimaji huondoa mlundikano
wa chumvi mwilini, husafisha kibofu cha mkojo pamoja na figo. Hii ina
maana kwamba juisii hii ni kinga tosha dhidi ya magonjwa ya kibofu cha
mkojo na figo.
KAROTI+EPO+PEASI+EMBE
Juisi ya mchangayiko wa karoti, epo, peasi na embe hushusha joto la
mwili, huondoa sumu mwilini, hushusha shinikizo la damu na hupambana na
matatizo ya kupumua.

PAPAI+NANASI+MAZIWA
Mchanganyiko wa papai, nanasi na maziwa, ambao una kiwango kikubwa
cha vitamin C, E na Chuma (Iron), huboresha rangi ya ngozi na kuifanya
iwe nyororo na husaidia mmeng’enyo wa chakula tumboni (metabolism).
NDIZI+NANASI+MAZIWA
Nao mchangayiko wa ndizi, nanasi na maziwa una vitamin nyingi na virutubisho vingi na huondoa tatizo la ukosefu wa choo.
Kwa ujumla, juisi ya mchanganyiko wa matunda hayo ukitumiwa kama
ipasavyo hutoa kinga tosha dhidi ya magonjwa mbalimbali ya mwili na
huweza pia kuwa tiba ya magonjwa yaliyotajwa hapo awali. Ili uone faida
za matunda katika suala zima la afya ya mwanadamu, jenga mazoe ya kula
matunda hayo kabla hujapatwa na maradhi, kwani kwa kufanya hivyo utaupa
mwili wako ile kinga yake ya asili ya kupambana na adui maradhi.
Comments
Post a Comment