Katika
makala hii tutajifunza mengi kuhusu Aleji au mzio kwa Kiswahili zaidi. Tutaona
uhusiano uliopo baina ya upungufu wa maji mwilini na ugonjwa wa aleji na ikiwa
utanielewa basi utakuwa umeelewa namna ya kujikinga au kujitibu na ugonjwa huu
ambao unasumbua watu wengi sana.
Mwaka
2006 mpaka 2007 nilikuwa nikisumbuliwa sana na aleji ya vumbi. Wakati huo
nikipita barabara ya vumbi ilikuwa lazima nijifunike pua maana kama gari
ingepita karibu na kunitimulia vumbi basi ningepiga sana chafya na hata
kukohoa, lakini nilipojuwa uhusiano wa aleji na upungufu wa maji mwilini na kuanza
kuyanywa ndipo nilipoona kitu kigeni kinatokea.
Ni kuwa ndani ya mwezi mmoja tu tangu nianze kuifuatilia tiba kwa kutumia maji basi aleji hiyo ya vumbi ilipotea kiasi kwamba hata ukitupa vumbi moja kwa moja kuja usoni kwangu hakuna chochote ambacho kinatokea iwe ni chafya au kikohozi.
Ni kuwa ndani ya mwezi mmoja tu tangu nianze kuifuatilia tiba kwa kutumia maji basi aleji hiyo ya vumbi ilipotea kiasi kwamba hata ukitupa vumbi moja kwa moja kuja usoni kwangu hakuna chochote ambacho kinatokea iwe ni chafya au kikohozi.
Aleji
katika lugha nyepesi kabisa ni kitendo cha mwili kupungukiwa maji wakati
histamini inapozarishwa kupita wastani ili kuhimiza unywaji wa maji na
ugawanywaji wa kiasi kidogo cha maji kipatikanacho mwilini.
Histamini
ni kihisio cha kwanza (primary sensor) cha ubongo kinachozarishwa ili
kujishughurisha na ugawanywaji wa maji kwa viungo mhimu wakati kunapokuwa na
upungufu wa maji mwilini. Inajihusisha na kazi ya ugawanywaji wa kiasi kidogo
kinachopatikana cha maji (maji ya mgawo kutokana na wewe kuendelea kusubiri kiu
ndipo unywe maji) wakati wa upungufu wa maji mwilini (Unintentional chronic
dehydration).
Histamini
katika lugha rahisi:
Histamini
ni kemikali ambayo miili yetu huitoa inapohitaji msaada kusawazisha upungufu wa
vitu mhimu sana mwilini kama maji, chumvi au potasiamu. Histamini na wasaidizi
wake wengine watano (5 buddies) watasaidia kuusawazisha upya mwili ambao upo
nje ya usawa. Kwa hakika Histamini ni kitu kizuri ambacho huokoa maisha yetu
kwa mujibu wa Dr. Batmanghelidj.
Sababu
ya kutokuelewa namna hasa histamini inavyofanya kazi mwilini, dawa
zimetengenezwa kuidhiti. Wakati histamini imezarishwa, yaweza kuendelea
kuzarishwa na kuzarishwa kwa sababu tunakula au kunywa kitu kimoja ambacho
miili yetu haiwezi kukitumia.
Mfano
mzuri ni juisi ya chungwa. Juisi ya chungwa huwa na kiasi kingi cha potasiamu
ambayo miili yetu haiwezi kuitumia bila uwepo wa chumvi. Kujifunza mengi kuhusu
chumvi na umhimu wake mwilini bonyeza hapa =>
Kwahiyo, inapotokea mtu anakunywa juisi ya chungwa na hatumii kiasi kinachostaili cha chumvi ili kuiwezesha potasiamu kuziingia seli za mwili, basi histamini hutolewa kurekebisha tatizo hilo. Kila mtu anahitaji 3/4 gramu za chumvi kwa kila 250 ml za juisi ya chungwa ili potasiamu iliyomo kwenye chungwa iweze kutumika na seli za mwili.
Kwahiyo, inapotokea mtu anakunywa juisi ya chungwa na hatumii kiasi kinachostaili cha chumvi ili kuiwezesha potasiamu kuziingia seli za mwili, basi histamini hutolewa kurekebisha tatizo hilo. Kila mtu anahitaji 3/4 gramu za chumvi kwa kila 250 ml za juisi ya chungwa ili potasiamu iliyomo kwenye chungwa iweze kutumika na seli za mwili.
Katika
kitabu kiitwacho‘’ABC of Asthma, Allergies and Lupus’ kilichoandikwa na Dr.
Batmanghelidj , ukurasa wa 149 chini na juu ya ukurasa wa 150, Dr.
Batmanghelidj ameandika: “Ni sera nzuri kuongeza kiasi cha chumvi katika juisi
ya chungwa ili kusawazisha matendo ya sodiamu na potasiamu katika kuhimili
ujazo unaotakiwa wa maji ndani na nje ya seli.”
Katika
baadhi ya tamaduni, chumvi huongezwa katika matikiti na matunda mengine ili
kukazia utamu wa matunda hayo. Kwa ujumla, matunda haya mengi huwa na potasiamu
tu kwa sehemu kubwa. Kwa kuongeza chumvi kabla ya kuyala, usawa kati ya
uchukuwaji wa sodiamu na potasiamu hupatikana. Jambo hili lapaswa kufanyika pia
kwa matunda mengine. Ni mhimu pia kuongeza kiasi kidogo cha chumvi katika juisi
unayotengeneza nyumbani na hata katika keki.
Kile
ulikuwa hujuwi labda hadi sasa ni kuwa tunahitaji chumvi kwa kila tunachokula
kwa sababu ya potasiamu. Potasiamu inapatikana karibu katika kila kitu
tunachokula. Ndiyo, CHUMVI yaweza kuwa MBAYA kwetu ikiwa hatunywi maji ya
kutosha kila siku ili kusawazisha ulaji huo mwingi wa chumvi.
Moja
kati ya matatizo makubwa siku hizi ni kuwa watu hatunywi maji ya kutosha.
Badala yake tumehamia kwa kahawa, chai, soda, pombe na kadharika. Mwili wa binadamu
unahitaji maji halisi na chumvi.
Uthibitisho wa hili ni matumizi ya madripu ya maji chumvi (SALINE IV’s) katika mahospitali na magari ya kukimbizia wagonjwa mahututi (ambulances).
Uthibitisho wa hili ni matumizi ya madripu ya maji chumvi (SALINE IV’s) katika mahospitali na magari ya kukimbizia wagonjwa mahututi (ambulances).
Madaktari
kamwe hawampi mgonjwa dripu la maji matupu, bali lenye chumvi ndani yake. Lita
moja ya dripu la maji huwa na chumvi gramu 9. Ukiwa mahututi katika ambulance
hupewi kahawa, Madaktari watakutundikia dripu la maji chumvi na wakati mwingine
watakutundikia lita nyingine ya vitamini, madini au dripu la maji sukari (dextrose
or glucose).
Mdhibiti
mzuri kabisa dhidi ya histamini ni chumvi. Ikiwa unakunywa maji mengi kila siku
na hautumii chumvi ya kutosha katika vyakula unavyokula au hata kuitafuna
chumvi yenyewe kwa ajili ya maji hayo mengi unayokunywa, mwili utaizarisha tena
histamini. Unaweza kulithibitisha hili wakati unapopatwa ghafla na chafya
kubwa, au kujisikia kama koo linaziba hivi na msongamano katika pua au koo kwa
ujumla. Ikiwa unalazimika kukohoa (au kubanja) ili kusafisha koo lako kila
mara, ni ishara unapungukiwa chumvi mwilini.
Hali
hii pia hutokea wakati tunakula vyakula au kunywa vinywaji vyenye potasiamu
nyingi (hivi mara nyingi ni vile vyakula vya kwenye makopo au maboksi vya
madukani) na bila kutumia chumvi nyingi kwa ajili ya potasiamu ya kwenye
vyakula au vinywaji hivyo. Utapata chafya kubwa na ya ghafla au kujisikia
msongamano katika mapafu au koo lako.
Chumvi
nyingi kuzidi pia itasababisha kuzarishwa kwa histamini na utapatwa na chafya
ya ghafla, msongamano mapafuni au kooni kama ilivyofafanuliwa hapo juu. Macho
ya mtu yaweza pia kuonesha wakati histamini imezarishwa mwilini kwa kutoa maji
maji (runny eye).
Unapokunywa
maji na unapatwa na dalili mojawapo kama hizo hapo juu, basi utatakiwa kuweka
kiasi cha chumvi katika ulimi wako na dalili zinapaswa kuwa zinapotea.
Ikiwa
unakula chakula na ukapatwa na dalili mojawapo hapo juu, utahitaji chumvi zaidi
kwa ajili ya potasiamu. Weka tu kipande cha chumvi mwanzoni mwa ulimi wako na
ikiwa dalili hizo (kupiga chafya kubwa, msongamano kooni au mapafuni au kwikwi)
zinatulia, utathibitisha kuwa unachokisoma hapa ni sahihi. Kujaribu hakuwezi
kumuumiza mtu.
Hauhitaji
kumeza chumvi, iache tu kama vile unavyomung’unya pipi juu ya ulimi wako kwa
dakika moja au mbili na kisha unaweza kuisafisha na maji kwenda chini au iteme
na uiweke pembeni.
Histamini
ni nini? ((medical): Histamine is a chemical substance that is given out in the
body in response to an injury or an allergy – Oxford Advanced Learners
Dictionary 8th edition).
Ikiwa
umetumia chumvi kuzidi au umeweka chumvi juu ya ulimi na ukapatwa na dalili
mojawapo hapo juu, basi utakunywa kikombe kimoja cha maji au viwili na dalili
zinapaswa kuwa zinatoweka.
Kila
mmoja anahitaji kuzijua ishara zake na kujaribu kupata usawa mahususi wa maji
kwa chumvi vivyo hivyo kwa kiasi mahususi cha chumvi kwa chakula anachokula.
Mdhibiti
mwingine mkuu kabisa tuliye naye mwilini mwetu dhidi ya histamini ni
adrenalini. Adrenalini hutolewa na mojawapo ya tezi mbili za adreno (adrenal
grands) zipatikanazo juu ya figo.
Kahawa
au kafeina, ndicho kitu kinachoweza kuisisimuwa tezi ya adreno kuitoa
adrenalini. Kaffeina pia itasababisha mwili kuitumia hifadhi yake ya nguvu
ambayo mwili huihitaji wakati wa kushughurikia matendo ya dharura (emergency).
Ikiwa hifadhi ya nguvu ya dharura inatolewa wakati hakuna udharura, mwili
utajikopa wenyewe kile unachokihitaji wakati wa dharura na hivyo kujihakikishia
uwezo wakati wa dharura nyingine.
Kaffeina
itapelekea mwili kujila au kujitafuna wenyewe (cannibalize off itself). Kila
seli ndani ya mwili inahitaji maji na chumvi ili ziwe seli zenye afya ambazo
zitafanya kazi pamoja kumuweka mtu katika afya bora.
Matumizi
ya vidhibiti vya histamini vya kibiashara, yataendelea kuuacha tu mwili na
upungufu wa maji na chumvi. Hebu fikiri tu kwanini madaktari wanatuambia tuwe
mbali na chumvi na sodiamu kwa sababu si vitu vizuri kwetu. Madaktari wanasema
tunapata chumvi nyingi kuzidi katika vyakula vyetu siku hizi.
Muombe
Daktari au muuguzi wako akuelezee kwanini wanatoa madripu ya maji chumvi kwa
wagonjwa mahututi wakati wanakuambia unapata chumvi nyingi kuzidi katika
chakula chako siku hizi?.
Tatizo
letu siku hizi hatunywi tena maji halisi ya kutosha. Tumegeukia vinywaji vya
kibiashara.
Wanyama
katika bustani za wanyama hunywa maji halisi na wakati mwingine husafiri umbali
mrefu zaidi kutafuta tu maji. Mbwa na paka wengi hawapati chumvi ya kutosha
siku hizi ndiyo maana ukimsogelea mbwa au paka cha kwanza atataka kukulamba
ngozi yako, ni kwa sababu ya chumvi iliyo juu ya ngozi yako. Inashauriwa
uongeze kiasi cha chumvi katika maji yao unayowapa kunywa na utaona mabadiliko
makubwa kwa wanyama wako.
Kwanini mwili unapatwa na aleji au mzio?:
Histamini
ni kemikali wakala wa ubongo mwenye kazi dhidi ya bakteria, virusi na mfumo
wakinga ya mwili dhidi ya maadui wa nje, kwa kuongezea inajihusisha pia na kazi
ya ugawanywaji wa maji mwilini.
Wakati
wa kiasi cha kawaida cha maji mwilini, yaani unapokuwa
unakunywa maji ya
kutosha kila siku, shughuli hizi (za kumonita bakteria, virusi, kinga ya mwili
na usambazaji maji) zinabaki tulivu au hazitengenezwi. Wakati upungufu wa maji
(dehydration) unapobaki kwa muda mrefu, Ubongo unaamuru uzarishwaji mwingi wa
histamini kuvutia uchukuaji wa maji.
Mfumo
huu wa histamini wenye seli utazarisha kiasi kingi cha transimita nyurolojia
(neurotransmitters).
Ni
kitendo hiki cha uzarishwaji mwingi wa histamini kinachotoa picha au majibu
kuwa una Aleji katika maabara.
Aleji
inapaswa kutibiwa na ongezeko la kiasi cha unywaji maji. Kwa wastani hali hizi
zinapotea baada ya siku tatu hadi wiki nne za urekebishwaji wa ongezeko la
unywaji maji.
Uzarishwaji
wa histamini utapunguwa wenyewe kwa ongezeko la unywaji maji.
Kitu
kingine mhimu wakati unaendelea kuyarudishia maji taratibu mwilini mara baada
ya kukutwa una Aleji ni vitamin C. Ni mhimu kutumia vyakula, matunda, mboga za
majani na juisi zenye vitamin c kwa wingi na hapa napendekeza juisi ya ubuyu,
kitunguu swaumu, unga wa mlonge na matunda karibu aina zote. Ni kwa sababu
vitendo vile viletwavyo na aleji huathiri pia kinga ya mwili kwa kiasi kikubwa
sana.
CREDIT
: MITANDAO MBALIMBALI
thanx
ReplyDeleteReading this in 2017. Thanks.
ReplyDelete