Skip to main content

Faida za tunda la karoti



Faida ya matumizi ya zao la karoti pamoja na faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa zao hilo, ambalo kimsingi mizizi yake ndiyo hasa zao lenyewe.

kumbuka kuwa karoti inalimwa karibu kila pembe ya dunia hii. Zao hili linatofautiana katika rangi, kwani kuna karoti nyeusi, zenye rangi ya pinki, nyekundu na njano. Karoti yenye rangi nyekundu na njano ndiyo hasa tunayolima hapa TZ. Karoti za rangi nyekundu na njano ndizo zinasemekana kuwa na virutubisho vingi sana kuliko karoti nyingine.



Karoti ina protini kidogo na haina mafuta kama tulivyoona kwa tunda la avocado. Pia ina asili ya wanga, na ni chanzo kizuri cha vitamini B, C na E. Aidha ina madini mengi ikiwemo madini ya chuma. Kuna kitu kinaitwa beta-carotene ambayo imo ndani ya karoti na hii ikiingia mwilini inabadilishwa na kuwa vitamini A. Vile vile karoti ina kirutubisho kinachoitwa fiber ambacho ni muhimu kwa kukinga kuta za utumbo.

Karoti ikitumiwa vizuri na tena mara kwa mara inasaidia kukinga na kuponya magonjwa yafuatayo: macho hasa kutoona gizani au kwenye mwanga hafifu, ngozi, kupunguza tindikali inayodhuru tumboni na kukinga magonjwa yenye asili ya kansa.



Karoti inaweza kuliwa kwa namna mbalimbali kama vile, ikiwa mbichi kwa kutafuna, inaweza kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga zingine, inaweza kusagwa na kupata juisi ambayo pia inaweza kuchanganywa na juisi zingine, aidha kukatwakatwa na kuchanganywa kwenye salad ya matunda au mbogamboga. Machicha ya karoti iliyosagwa yanaweza kutumika kama dawa kukinga ama kuponya maradhi ya nje ya mwili.
 IMETAYARISHWA  NA  NEEMA  HERBALIST  BLOGU

Comments

Popular posts from this blog

IJUE SAYANSI YA KUSIMAMA KWA UUME

Ukosefu  na/ama  upungufu wa  nguvu  za  kiume, ni tatizo linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume duniani. Tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume ni  nini  ? Ukosefu  ama  upungufu  wa  nguvu za  kiume  ni  ile  hali  ya  mwanaume  kutokuwa  na  uwezo  wa kufanya  tendo  la  ndoa  kwa  ukamilifu HATUA  MBILI  MUHIMU  KATIKA  KUSIMAMA  KWA  UUME Ili  mwanaume   aweze  kufanya  tendo  la  ndoa  na  andelee  kufanya  tendo  la  ndoa, ni  lazima  uume wake  upitie  hatua  kuu  mbili  kama  ifuatavyo : Hatua  ya  kwanza , ni  lazima  uume  wake  uweze  kusimama  barabara  na...

TIBA YA ASILI YA KUACHA PUNYETO KWA WANAUME

Pilipili  Mbuzi Punyeto  ( kwa  wanaume  )  ni  kitendo   cha  mwanaume, kujifikisha  mwenyewe  kileleni  kwa  kujichua  uume  hadi  kumwaga  mbegu  za  kiume.  Uchunguzi  unaonyesha  katika  watu  wa  jinsia  ya  kiume  kumi  wenye  umri  wa  kuanzia  miaka  16  hadi  45, angalau  wanne  kati  yao  wamewahi  kupiga  punyeto  katika  kipindi  fulani  cha  maisha  yao, na  wawili  kati  yao  wanajihusisha  na  upigaji  punyeto. Uzoefu  unaonyesha, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wanao  piga  punyeto  huanza  katika  umri  wa  kubalehe  ( miaka  14-16  ), wengine  huachana  na  tabia  hiyo  mara  baada  ...

FAIDA KUMI ZA MTI WA MKOMAMANGA

Mti   wa   Mkomamanga   ni   mti   wenye   faida   nyingi   sana   katika   afya   ya   mwanadamu. Mti   huu   una   virutubisho –afya     mbalimbali   ambavyo   ni   muhimu   katika   afya   ya   mwanadamu.   Virutubisho   hivyo   vinapatikana   kwenye   magome, majani, mbegu, maganda   ya   matunda, juisi   ya   matunda   pamoja   na kwenye   maua   ya   mti   wa   mkomamanga. Zifuatazo   ni   faida   muhimu   za   mti   wa   mkomamanga : 1.           Maganda   ya   tunda   la   mkomamanga   yakichemshwa    hutoa   juisi    ambayo   hutumika   kama   dawa   ya   kufunga   kuhara. 2.   ...