Mkazi mmoja wa
Manispaa ya Mtwara Sharifu Issah maarufu kamaZamda Salumu amefikishwa
mahakamani kwa kosa la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya
mwanamke na kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa na kuishi pamoja kama
mke na mume.
Akisoma kesi hiyo
hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha
157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria iliyofanyiwa marekebisho mwaka
2002.
Kabate amedai kuwa
mshtakiwa kati ya mwezi Machi mwaka huu na mwezi wa Juni akiwa katika vijiji
vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya Nanyambamkoa wa Mtwara kwa makusudi
alijifanya mwanamke na kumshawishi Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na
kufunga nae ndoa isiyo halali.
Hata hivyo hakimu
Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa
watu wa jinsia moja ya kiume kuishi kinyumba.
Mshtakiwa aliposomewa
shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi amekana shitaka hilo na
upelelezi wa kesi hiyo unaendelea mshtakiwa amerudishwa mahabusu na kesi hiyo
itatajwa mahakamani hapo Septemba 28, 2017
CREDIT : EATV
Comments
Post a Comment