JESHI la Polisi Mkoa
wa Singida linamshikilia mlemavu
wa miguu anayejishughulisha na ufundi
wa viatu na
bajaji mjini hapa, Khalid Rjab (
45 ), kwa tuhuma za
mauaji ya mtu anayedaiwa kuwa ni mgoni
wake, aliyemfumania ndani ya
chumba nyumbani kwake.
Fundi huyo anadaiwa kumuua kwa
kumchoma kisu sehemu
mbalimbali mwilini mwake ikiwamo
kifuani, Iddi Selemani ( 40 )
kwa madai ya
kumfumania akiwa na mkewe
tena chumbani kwake
wakifanya mapenzi.
Tukio hilo lilitokea juzi saa
9;30 mchana, katika eneo la
Jineri.
Inadaiwa kuwa Selemani
aliwahi kuonywa juu
ya tabia hiyo na
kutakiwa aachane na
mwanamke huyo Mariam Ibrahim ( 25 )
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Singida, Isaya Mbughi, aliwaambia waandishi wa
habari kuwa Selemani alikutwa chumbani ndanu ya
nyumba ya mlemavu
huyo na alipotaka
kukimbia alishikwa mguu
kisha kuangushwa chini
na kuchomwa kisu.
Alisema Selemani, aliyekuwa
anajishughulisha na usagaji
nafaka, alifarika dunia muda
mfupi baada ya
tukio hilo akiwa njiani kupelekwa
Hospitali ya Rufani ya
Mkoa wa Singida kwa
ajili ya matibabu, kutokana na
kuvuja damu nyingi.
Kutokana na tukio
hilo,Kamanda Mbughi, alisema
Khalid anashikiliwa na polisi
pamoja na mkewe Mariam.
Aidha , Kamanda Mbughi amewataka
wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi pale
wanapokuwa wamekosewa badala
yake washirikiane na
jeshi hilo ili
kutokomeza vitendo hivyo.
Mbughi alitoa wito
pia kwa wanandoa kulinda
heshima zao ili kujenga imani kwa
kila mmoja badala ya
kujiingiza katika vitendo vya
uasherati .
Kutokana na kifo
cha kijana huyo, Balozi wa
mtaa huo, Christian Khwere
ameahidi kuitisha mkutano ili kuzungumza
na vijana juu ya kujihusisha
na mapenzi dhidi
ya wake za
watu.
Mwili wa Selemani
ulisafirishwa jana kwenda
kijijini kwao, Kisiluda wilayani Ikungi kwa
ajili ya mazishi.
CREDIT:
GAZETI LA
NIPASHE, JUMAPILI SEPTEMBA 17,
2017.
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment