Msanii wa bongo fleva, Linah Sanga amefunguka na kudai
hakuwa amejipanga kwa kipindi hiki kuwa na mtoto ila anamuomba Mungu isiwe
kigezo cha yeye kupotea katika muziki ili aje kuwa mfano kwa wasanii wenzake wa
kike wanaogopa kubebea ujauzito.
Linah amebainisha hayo kupitia kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE
'FNL' kutoka EATV baada ya kuwepo imani kwa baadhi ya watu wakidai msanii
akioa, akiolewa hata akijifungua na mtoto mara nyingi hawezi kuendelea kufanya vizuri
katika kazi zake kwa kuwa majukumu ya ulezi yanaongezeka na kupelekea kupotea
katika 'industrial' ya muziki.
"Nina muomba Mungu usiku na mchana nisije kupotea
katika 'game' kwa sababu ya uzazi, ili iwe mfano hata kwa wengine ambao
watakuja nyuma yangu, labda wanaogopa kuzaa kwa kufikiri watapotea. Ila mimi
nafikiri ni jinsi mtu mwenyewe anavyoishi na mashabiki zake", amesema Linah.
Pamoja na hayo, Linah ameendelea kwa kusema "Sikuwa
nimejipanga kupata mtoto katika kipindi hiki ila nilikuwa na-wish nipate
ujauzito nizae lakini sikufahamu ni lini itanitokea hivyo. 'So' kipindi kile
nilichokuwa na-wish nikawa kila nikijaribu haingii, nikajisahau na kujikuta
imekuja hata sikutarajia, lakini kwa kuwa nilikuwa nina uhitaji nikasema hakuna
neno. Japo nilishauriwa vitu vingi sana mwanzoni lakini nikasema hapana kwa
kuwa nimetaka kuzaa acha nifanye hivyo", amesisitiza
Linah.
Kwa upande mwingine, Linah amesema kwa anajipa mapumziko
katika kufanya kazi zake na kuwataka mashabiki zake wamvumilie mpaka mwakani
(2018) katika miezi ya mwanzoni ndipo atakapoachia kazi yake mpya
CREDIT : EATV
Comments
Post a Comment