MWANAUME KUMHUDUMIA MWANAMKE NI SEHEMU YA NGUVU ZA KIUME, DADA YANGU ACHA KUWA MWANAUME!
Mrembo mmoja, kupitia ukurasa
wake wa facebook, ameweka ujumbe
unao wataka wanawake
wenye tabia ya
kuwahonga na kuwahudumia
wanaume zao, kuacha mara
moja tabia hiyo kwa madai ya
kwamba, kuhonga na kumuhudumia
mwenza ni jambo
linalopaswa kufanywa na
mwanaume na sio
mwanamke.
Maelezo ya mwanadada
huyo, yanasomeka kama ifuatavyo :
Hii ni Dada zangu ambao mmegeuka wanaume katika mahusiano
yenu, mnapaswa kujua kuwa hakuna mwanaume ambaye napenda kuoa mwanamke ambaye
anamhudumia.
Hapa mnielewe sio mwanmke ambaye anamzidi kipato hapana,
unaweza kumzidi kipato mume wako lakini usimhudumie, kwamba kuna wale wanaume
ambao;
Anaendesha gari la mkewe, anaomba hela ya chakula kwa mke,
wazazi wakiumwa ni mke, ada ni kutoka kw, akitaka kutoka out ni mke yaani hata
kama anafanya kazi lakini hachangii kitu katika familia. Na kama ni mpenzi wako
tu hata si mume basi wewe hajawahi kukupa hata hela ya Pedi lakini kila akiwa
na shida ni kukulilia.
Tena kama mwanamke
ambaye anaomba hela ya saluni ambaye ukimnyima ananuna, yaani una boyfriend
anakuomba hela ukimnyima ananuna.
Dada yangu jua huyo hatakuja kukuoa, narudi
hatakuja kukuoa na kama ikatokea bahati mbaya akakuoa narudia kama itatoke
bahati mbaya naruidia tena kama itatoke bahati mbaya atakuoa basi jua kuwa utakua
na msaidizi tu.
Kwamba mwanaume kumhudumia mkewe au mpenzi wake ni sehemu ya
nguvu za kiume, kwamba huwezi kujiita mwanaume mbele za watu kama kila kitu
unamtegemea mkeo, maamuzi yote ni mke. Sasa ili uwe na kauanaume hata kambali
ni lazima uwe na kamchepuko flani ambako unakahonga, ambako kanakuambia Pedi
zimeisha, kana shida ya hela ya saluni na ambako kanaweza kununa ukikanyima
hela.
Ndiyo ilivyo hili ni suala la kisaikolojia upende usipende
hivyo Dada yangu hembu acha upumbavu, narudia acha upuuzi wa kuhonga honga
wanaume.
Hapa mnielewe kusaidiana na mpenzi wako ni raha na ni kitu
kizuri sana, kwamba kama ukiwa na shida anakusaidia bila kusitasita basi hata
yeye akiwa na shida msaidie.
Kama yeye anakununulia kitu na kukupa zawadi bila hata
kuombwa na wewe fanya hivyo hayo ndiyo mapenzi.
Lakini Dada yangu kama ukimuomba vocha ya buku atakuambia
matatizo mpaka ya marehemu Bibi yake, hakupi au unaomba vocha leo halafu
anakupa baada ya mwezi huyo hata akilazwa Hospitalini usimnunulie panado.
Kwanza ni mwanaume
gani huna hata hela ya vocha halafu unatafuta wanawake, kwani sabuni ziko wapi,
nenda kanunue JAMAA kama watoto wenzako.
Sasa mimi nishachoka kuandika, sasa wewe jifanye unapendwa
unachukua mpaka na mkopo eti kuhudumia mwanaume mtu mzima na midevu yake, eti
anakudnaganya anasoma yuko chuo umlipie! Pumbavu yaani umlipie mwanaume ada,
unaakili Dada yangu! Kwani Baba yake yuko wapi, aende akafanye kibarua kama
wanaume wenzake ajisomeshe. Sasa wewe lipa ila ukishadhulumiwa ukachwa
unakaribishwa kusoma na Kitabu changu!
MAKALA
NYINGINEZO
JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment