Mwanamke
aliyetajwa kuwa mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki
Mwanamke raia wa Misri ambaye
aliaminiwa kuwa mtu mwenye uzani mkubwa zaidi duniani amefariki kwenye
hospitali moja katika umoja wa falme za kiarabu
Eman Ahmed Abd El Aty alikuwa amepelekwa nchini India
kufanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wa mwili.
Vyombo vya habari viliripoti kuwa alikuwa amepunguza
uzito kwa kilo 300 kutoka kwa uzito wa kilo 500 lakini akafariki kutokana
matatizo mengine ya kiafya.
Taarifa za hospitali zinasema kwa mwanamke huyo mwenye
umri wa miaka 37 alikuwa na ugopnjwa wa moyo na matatizo ya figo.
"Tunatuma rambi rambi na maombi yetu kwa
familia," taarifa ya hosptali ilisema
Bi Abd El Aty amekuwa kwenye hospitali huko Abu Dhabi tangu
mwezi Mei baada ya kuhamishiwa huko kufuatia upasuaji aliofanyiwa nchini India.
Kabla ya hajafanyiwa upasuaji familia yake ilisema
kuwa hakuwa ameondoka nyumbani kwake kwa miaka 25.
Kutokana na hali kwamba hakuwa ametoka kitandani kwa
miaka 25, kulikuwa na hatari kwake kuugua maradhi ya kupumua na ili
kusafirishwa madaktari walichukua tahadhari kubwa na kumpa dawa za kuyeyusha
damu mwilini.
Kitanda alichosafirishwa nacho ni kitanda maalum kilichoundwa na
mafundi wa Misri kwa kufuata matakwa ya shirika la ndege la EgyptAir.
Kilikuwa na mitambo na vifaa vya huduma ya dharura.
Familia ya Eman Ahmed inasema kuwa alikuwa na uzani wa
kilo 5 alipozaliwa kabla ya kupatikana na ugonjwa wa matende, ugonjwa ambao
unasababisha kufura kwa mwili kutokana na maambukizi ya vimelea.
Wakati alipofikisha umri wa miaka 11, uzani wake
uliongezeka maradufu na akaugua kiharusi ugonjwa uliomuacha kitandani kwa
kipindi kirefu cha maisha yake.
Baada ya kampeni kupitia mitandao iliyofanywa na dada yake,
aliweza kusafiri hadi mjini Mumbai kupata msaada wa madakatari wa India.
Hata hivyo alihamishwa tena kutoka India baada ya
familia yake kutofautiana hadharani na madaktari wa India.
CREDIT : BBC
SWAHILI
Comments
Post a Comment