Nilihangaika sana na mke wangu kupata
mtoto siku za nyuma, lakini miaka 7 iliyopita Mungu akatujalia mtoto mmoja wa
kike na mpaka leo hatujafanikiwa kupata mtoto mwingine, nampenda sana kwani ni
furaha yangu maishani, lakini juzi rafiki mkubwa wa mke wangu aliniita faragha
na kuniambia mtoto huyo sio wangu ni wa mzee mmoja jirani yetu. Nimepatwa na
mshtuko mkubwa na ni siku ya tatu leo sijaenda kwenye biashara zangu na
sijamuuliza mke wangu lolote mpaka sasa. Embu nisaidieni ushauri moyo unaniuma
sana.
CREDIT : EATV
Comments
Post a Comment