MWANAMKE MWENYE MATATIZO YA AKILI AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA, LAKINI AKUTWA NA PACHA MMOJA TU. KILICHOTOKEA KWA PACHA MWINGINE, KITAKUSIKITISHA
Tukio hili lililo vuta hisia za watu wengi limetokea siku ya Jumamosi ya tarehe 09 Septemba 2017 katika viunga vya makutano ya barabara za Ikoya na Okitipupa huko jijini Lagos nchini Nigeria.
Taarifa zinasema mwanamke huyo ambae mpaka sasa jina lake bado halijajulikana alikutwa akiwa amejifungua katika eneo la jalala ambalo hulitumia kama makazi yake na kuvuta idadi kubwa ya watu ambao walishikwa na huruma na kuanza kufanya jitihada mahsusi ili kuokoa maisha ya mwanamke huyo pamoja na kichanga chake.
Jitihada za wasamaria hao zilizaa matunda ambapo taarifa zilimfikia mwenyekiti wa serikali za mtaa wa eneo hilo aliyejulikana kwa majina ya Morenike Alaka, ambae wakati wa tukio alikuwa akihudhuria halfa iliyo andaliwa na First Lady wa Gavana wa jimbo la Lagos, Arabrin Betty Anyanwu – Akeredolu.
Morenike Alaka baada ya kupata taarifa hizo haraka aliondoka katika hafla hiyo na kufika katika eneo la tukio kwa ajili ya kufanya taratibu za kuokoa maisha ya mama na mtoto wake.
Kama mwanamke na mama aliyeguswa na tukio hilo , baada ya kufika katika eneo hilo aliwaagiza madaktari na wanausalama wa mtaa wake kufika katika eneo hilo upesi sana ili kumchukua mtoto huyo kwa ajili ya uangalizi na matibabu zaidi.
Inaelezwa kuwa, baada ya madaktari na wanausalama kufika katika eneo hilo, mwanamke huyo alikataa kumtoa mtoto wake na kutishia kumuua mtoto kama watu hao watamchukua.
Mwanamke huyo aliendelea kuongea mbele ya umati ulio kusanyika katika hilo akisema kuwa, alijifungua mapacha lakini mtu mmoja alifanikiwa kumchukua /kumuiba pacha mmoja.
Baada ya takribani masaa kumi na kumsihi na kumshawishi mwanamke huyo hatimae walifanikiwa kumchukua na kuondoka nae hadi hospitali kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Taarifa zaidi zinasema mtoto huyo anaendelea vizuri hospitali.
CHANZO :
VYOMBO MBALIMBALI VYA HABARI
NCHINI NIGERIA.
MAKALA NYINGINEZO
JINSI KISUKARI
KINAVYO SABABISHA MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
JINSI KITAMBI KINAVYO
PATIKANA NA JINSI UNAVYO WEZA KUKIONDOA KWA
TIBA ASILIA
JINSI PUNYETO INAVYO
SABABISHA TATIZO LA UKOSEFU NA UPUNGUFU
WA NGUVU ZA KIUME
IJUE SAYANSI YA
NGUVU ZA KIUME
UHUSIANO KATI YA
UNENE ULIO ZIDI NA TATIZO LA UKOSEFU
NA UPUNGUFU WA NGUVU ZAP KIUME
KISA UGONJWA WA
KISUKARI MWANAMKE AMKIMBIA MUMEWE WA NDOA
NA KWENDA KUISHI NA JIRANI
KUTANA NA
MWANAMKE AIYE JITOLEA KUMTIBU
MUMEWE MARADHI YA AJABU
PUNYETO ILISABABISHA
NINUSURIKE KWENDA JELA
Comments
Post a Comment