Mlimbwende Tunda ambaye ni gumzo kwenye mitandao ya kijamii
kutokana na urembo wake, amekana taarifa za kutoa ujauzito ambao alionekana
nao, na kusema hakuwa na mimba na hajawahi kupata ujauzito maishani mwake
Akizungumza na
mwandishi wa East africa Television Tunda ambaye pia ni 'video vixen', amesema
tumbo alilonalo lilikuwa ni kitambi kilichoongezeka kutokana na kunenepa, na
kwa sasa anafanya mazoezi kuweza kurejesha mwili wake wa kawaida.
"Sina mimba na sijawahi kuwa mjamzito, hili tumbo
nimeongezeka tu nina asili ya tumbo nikinenepa na tumbo linaongezeka, hizo
tetesi za kutoa mimba ndo nazisikia kwako sijawahi kutoa mimba”, amesema Tunda.
Hivi karibuni mrembo huyo amekuwa akipost picha
zinazomuonyesha na tumbo kubwa, hali iliyoibua gumzo kwa mashabiki kuwa huenda
mrembo huyo anatarajia kupata mtoto.
CREDIT : EAST
AFRICA TELEVISION
Comments
Post a Comment